UCHAWI NA WATUMISHI WAKE.

Kitu uchawi ni kitu ambacho kipo katika jamii katika kila umma,na si vizuri mtu kupinga kuwepo kwa uchawi hapa duniani.Ndio maana inayamkinika kusema kuna watu wanaumwa maradhi yatokanayo na kufanyiwa uchawi yaani kurogwa.mchawi anaweza  kumroga mtu kwa chochote alichokusudia ila hakiwezi kumdhuru mpaka m/mungu akubali kuzudhurika huyo aliyerogwa.

   Na aliyerogeka asidhani m/mungu kashindwa kumkinga "La hasha" bali aone tu huo ni mtihani kwake tu.je atafanya njia ipi ili kujinasua na huo uchawi.

  Ikiwa atafuata njia sahihi  za kujiagua huo uchawi ambazo zimefundishwa  na mtume muhammad (s.a.w) itakuwa amefauru na mtihani huo wa kurogwa,pia itakuwa umempandisha daraja ya kiuchamungu kwa kuukubali  mtihani mzito kama huo.Au ikiwa atafuata njia za kishirikina za kuagua uchawi kwa uchawi hapo atakuwa amejiingiza mwenyewe motoni kwa kutoamini  njia sahihi alizofundisha mtume muhammadi (s.a.w) za kuagua huo uchawi.Hatari zaidi ni kwamba  endapo atatumia  njia za kishirikina nae badala ya kuwa ni mgonjwa tu atageuka pia kuwa mchawi  kutokana na  masharti ya kiuchawi ya matibabu atakayopewa na huyo mganga mchawi ili ayatekeleze,mfano kuoga dawa usiku wa manane uchi juu ya kaburi,kuzika vitu njia panda, pamoja na kujifunga vitu mwilini au kufungia  sehemu yeyote kama juu ya mti ,nyumba na sehemu nyinginezo.

  kuagua uchawi kwa uchawi ni haramu  hata kama utapona hiyo siyo hoja kama alivyoeleza mtume (s.a.w)

    Amesimulia jabir (R.A) kuwa mtume (s.a.w) aliulizwa  kuhusu kuondoa uchawi kwa uchawi alijibu "hiyo ni  Aamali ya  shetani".(Ahmad,Abuu Dau).

Jambo lingine ni kwamba uchawi unaweza kumuathiri mtu katika mambo mengi tu siyo  afya ya kiwiliwili tu kama wanavyodai watu wengi bali hata shughuri za kawaida kama biashara.Pia uchawi unaweza kufarakanisha ndoa au kumuharibia mtu masomo kwa kumtia mtu kasoro kwa kuchanganyikiwa awapo darasani na mambo mengi tu ikiwemo kutoona vizuri,kuumwa kichwa kwa kuwa wanaotumikia uchawi ni mashetani wa kijini humuingia mwanadamu na kushambulia kiwiliwili kwa kumtia maumivu ama kuisumbua akili yake naye akapuuza lenye kufaa na akang'ang'ania lisilofaa,kama mwanamke kudai talaka ghafla bila sababu za msingi au mume kuacha bila ya sababu  za msingi na hatimae wote hawa hujuta.Ama mtu kuacha kazi bila ya kukusudia au kuachishwa kazi bila ya sababu za msingi au kudhoofika biashara kwa kupotelewa na pesa au kuibiwa pesa kila siku hata zifungwe wapi,au kuchukiwa na wateja katika biashara yako bila ya sababu za msingi,ama mwanamke kutozaa bila ya sababu za kutomfanya asizae.

Pia mtu anaweza kuvurugukiwa akili mfano mwendawazimu hali vipimo vyaonyesha yuko timamu kiakili.

   Basi kazi hii yote hufanywa na mashetani wa kijini kwa kuwatumikia hao mabwana zao wanaowatuma kwa kuwaahidi ama kuwapatia zawadi mbalimbali na huku wakitarajia kuingia nao motoni kwa huo ubaya wanaoufanya 

  

     FAIDA YA KUJITIBU KWA KUTUMIA 

                     QUR'AN  TUKUFU.

 Ruqya ya kisheria ni kisomo anachisomewa mgonjwa (zinguo) kwa aya za quran au majina ya mwenyezimungu au sifa zake pamoja na dua mbalimbali alizofundisha mtume muhammad (s.a.w).Njia hii watu hupona sana na hupata faida kubwa kutokana na imani inayopatikana baada ya kuona matokeo  mazuri ya kisomo alichosomewa .Na jambo jingine  yeyote anayesomewa Ruqya lazima apewe taratibu za kudumu nazo za kiibada ambazo humzidishia uchamungu.Mambo mengine yawezayo kutokea baada ya kisomo ni kufunguka mafundo  mwilini au kumtembea vitu mwilini au kihisi joto  kali sana ama baridi kali sana ama baridi pamoja na kutapika   au kuharisha endapo mgonjwa anasumu  ya uchawi mwilini mwake,na mwanamke huenda akatokwa na damu nyingi ya hedhi kwa maana ya kusafisha kiwiliwili,au kutokwa na jasho jingi.Haya yote kwa vile hutokea bila ya kuchinja kuku  au njiwa au kunyweshwa majani yoyote kama ilivyozoeleka ,basi mgonjwa huzidi kujawa na imani kuhusu dini yake kwa faida anayoiona na huenda  akawa mchamungu kutokwna na kutokana na zoezi hili ,pia huandikiwa thawabu kwa vile amefuata tiba aliyoamrisha mola wake.Baadhi ya wengi huona ajabu kutibiwa kwa Qur'an mfano mtu aweza kuuliza "Hivi mtu kusomewa Quran tu anaweza ? Jibi ni kwamba yawezekana kwani quran ni dawa kama alivyosema mtume (s.a.w)

   kutokana na Rajaali ghanawiyyi(R.A) amesema;

     "Amesema mtume (s.a.w)jitibuni kutokana na alichojisia mwenyezimungu kabla hajasifiwa na viumbe wake .kwa kile alijisifia mwenyezimungu mwenyew .

  Alhamdulillah  na Qulhuwallaahu ahadu,na ambaye hakuponyeshwa na Quran hana ponyo tena kwake."

pia akasema tena mtume (s.a.w) kuhusu hiyo hiyo ruqya  yasheria.

  Amesema juu yake rehema na amani "si vibaya kufanya ruqya maadamu hakuna shiriki ndani yake, na mwenye kuweza kuweza kumnufaisha ndugu yake miongoni mwenu na afanye"-(muslimu)

     MATESO YA KUJITIBU KISHIRIKINA.

  Watu wenye desturi ya kujitibu kwa waganga washirikina yaani wachawi hupata mateso makubwa sana kutokana  na masharti wanayopewa na hao waganga kama vile kutembezwa uchi,kukalishwa masiku mengi bila ya kuoga,kuzuiwa kufanya tendo la ndoa,kubebeshwa mizigo kama vile Tarasimu au hirizi,kulishwa chakula chooni,kuziniwa na kuelezwa ndiyo masharti ya tiba ,kuchorwa mwilini hadi sehemu za siri,kutupa vitu majalalani au njia panda usiku wa manane na mengine mengi yenye karaha zaidi ya hayo.

    Jambo lingine kuwekewa masharti magumu kama wasiangalie maiti au wasiingie kaburini pamoja na kushika maiti.Wasile vyakula vya shughurini kama harusini au maulidini pamoja na khitma na shughuri nyinyinezo zenye mjumuiko wa watu wengi,na wakila wale pekeyao.Au kupangiwa kula baadhi ya vyakula na baadhi kuambiwa wasile.Kwa maana hii mtu aliyetibiwa kishirikini hata kama atapona kimwili,bado atakuwa anaumwa kifikra kutokana na majukumu mazito aliyobebeshwa.

  Hata hivyo wapo watu wengi ambao hutumia njia za kishirikina katika biashara zao nao hukumbana na mizigo mizito kama kuambiwa mkono waliopokelea pesa wasirudishe chenji kwa mkono huo huo bali wabadilishe.Na hii ni desturi ya waganga washirikina kutoa masharti magumu kwa wateja wao ili kuwatia imani,na yawezekana hizo shurti haziwi na lazima yeyote bali ni namna tu ya kuwachota akili (kuwazubaisha).

  Hali hii imezoeleka mpaka ikafikia watu  kupewa dawa bila ya masharti magumu huwa hawaamini na hawaridhiki,kwa hali hiyo waganga wamewafahamu wateja wao jinsi walivyo na ndipo wanapozidi kuwawekea masharti magumu,nao hufikia wakasema baada ya kuhudumiwa "kwa jinsi dawa zake zilivyokuwa na masharti magumu naamini tu nitapona".Haya ni baadhi tu ya mateso wanayopitia wale wanaokwenda kutafuta tiba au kutibiwa na washirikina.

    Niachie maoni yako hapo chini nami takufatilia nikushauri zaidi.


Previous Post Next Post

Contact Form