DAWA YA KUONDOA MICHIRIZI KWENYE NGOZI.

  Tatizo la michirizi kwenye ngozi linasababishwa na  mambo mengi kama vile unene uliopitiliza baada ya kujifungua,kupungua mwili ghafra,matumizi ya vipodozi vyenye kemikali na mengine mengi.

Ili kuondoa tatizo hilo tengeneza dawa ifuatayo itakusaidia sana.

Mahitaji,

>>Mafuta ya nazi

>>Kitunguu maji

>>Sukari ya vijiko vitano

Matayarisho,

Katakata kitunguu chako vipande viwili,kisha chukua  kipande kimoja na ukisage kiwe ujiuji alafu changanya na sukari.

Matumizi,

Chukua kile kipande kingine cha kitunguu  na uchovye kwenye mchanganyiko huo wa kitunguu na sukari kisha ufikiche sehemu yenye michirizi.

Fanyanzoezi hilo kwa dakika tano hadi  kumi kisha acha sehemu hizo zikauke.

Baada ya kukauka sehemu hiyo basi utaosha kwa maji ya kawaida  kisha utapakaa mafuta ya nazi.

Fanya zoezi hilo hili kila siku mara moja hadi utakapopata matokeo mazuri.

Unaweza kutumia dawa hii hadi siku 14.


Usikose kutembelea mitandao yangu ya kijamii  Facebook,instagram na youtube kwa ajiri ya kujifunza Elimu ya tiba mbalimbali  kupitia Mitishamba matunda na dua kupitia  Quran tukufu kwa kubofya Icon za mitandao hiyo hapo 👇👇👇chini.



Previous Post Next Post

Contact Form