FAIDA ZA MTI WA MBAAZI KATIKA TIBA.

          MTI WA MBAAZI;

Huu ndio mti mkuu katika miti yote katika ulimwengu wa Tiba.Umeitwa mti mkuu kutokana na matumizi yake katika tiba.Ndio mti wenye uwezo wa kutibu maradhi mengi yatokanayo na ushirikini (uchawi) pia hata maradhi ya kawaida.

     Mti huu unatumika sana na waganga pia hata wachawi katika kuleta madhara mbalimbali kwa wanadamu.Pia mti huu ndio ambao kama mchawi atakwenda kuwanga usiku kisha akawa anahitaji kupumzika,basi sehemu ambayo anaiamini kuwa itakuwa salama ni katika mti huu wa mbaazi.Mti huu una maruhani wakali na wenye nguvu wanaousimamia na kuulinda mti huu na hiyo ni kwa uchache wa sifa za mti huu sasa tuangalie faida za mti huu katika tiba.

      1.KUMUANGUSHA MTU MBAYA AU KUMGANDISHA KATIKA ENEO LAKO;

Kama unataka kumuangusha mtu anaekuja kukuchezea kichawi katika eneo lako au kumgandisha eneo lako,mfano sehemu ya biashara nyumbani n.k fanya hivi;

   Chuma majani 28 ya mti wa mbaazi kisha yaponde ponde tia maji alafu changanya na chumvi ya mawe kidogo,kisha mwagia maji hayo sehemu ya nyumba yako au eneo la biashara yako.pindi unapofanya hivyo tia nia yako juu ya kutaka atakayekuja eneo hilo kukucheze katika ile michezo ya kichawi basi agande eneo hilo au aanguke na kuanza  kusema siri ya kilicho mleta hapo.

  2.KUONDOA MIKOSI NA NUKSI KATIKA MWILI.

   Chukua majani ya mbaazi ya kutosha kisha yatwange twange ,kisha weka kwenye maji ya kuoga kisha tia nia yako ya kuondosha mikosi na nuksi katika mwili kisha koga maji hayo bila kuchanganya na sabuni yoyote ile.

  Utafanya hivyo kwa muda wa siku tatu mfululizo asubuhi na jioni.

  3.ANAYETAKA KUPENDWA AU KUPANDA CHEO KAZINI AU KUKUBALIKA KATIKA JAMII INAYOMZUNGUKA.

  Chukua kijiti cha mti wa mbaazi kilichotoa maua kikwangue magome yake,yale ya juu yaanike kisha yasage  upate unga wake .Unga huo tumia kwa kuchanganya kwenye mafuta yako ya kupakaa.Na pindi unapopakaa pakaa kwa nia ya kupata mvuto,au kupanda cheo, au kukubalika katika jamii.Basi utaona maajabu ya dawa hiyo inshaallah.

  4.ALIYELOGWA KWA KUZIONA SIKU ZAKE ZA HEDHI KWA MUDA MREFU.

   Chukua mizi ya mti wa mbaazi changanya na majani yake kidogo,kisha chemsha katika maji.Basi maji hayo tumia kwa kunywa kikombe kimoja asubuhi na jioni fanya hivyo kwa muda wa siku tatu mfululizo,lakini pindi unapotumia dawa hii tia nia kwanza ya kutaka kupunguza idadi ya siku za hedhi  inshaallah.

  5.KUTIBU KIGUGUMIZI.

   Chukua mzizi wa mti wa mbaazi kisha  uchemshe alafu mpe mgonjwa mwenye kigugumizi anywa kwa kutia nia ya kuondoa tatizo la kigugumizi.inshaallah kwa uwezo wa m/mungu tatizo hilo litakuwa ni lenye kuondoka.

   6.KUVUTA WATEJA KATIKA BIASHARA YAKO;

  Chukua majani 28 ya mti wa mbaazi kisha yaandike majina ya BARHATIHI kila moja kisha yaanike,tafuta na Ambali nyeupe ya baharini itwange kisha changanya na unga uliotwanga kutokana na majani ya mti wa mbaazi.Tumia kwa kuoga na nyingine choma sehemu ya biashara yako.Utaona maajabu makubwa ya dawa hiyo ishaallah.

  7.KUMGANDISHA MCHAWI ALIE NDANI AU NJE YA NYUMBA YAKO.

  Chukua majani ya mti wa mbaazi kisha changanya na chumvi ya mawe twanga twanga majani hayo kisha mwagia ndani au dekia,bila kusahau nia yako juu ya jambo hilo.

   Kama mtu mbaya yumo ndani ya nyumba yako hataweza kutoka kwenda nje kuwanga au kuroga na kama yupo nje hataweza kuingia ndani ya nyumba yako.Na akilazimisha kuingia ataganda eneo hilo na atoki.

   8.KUONDOA MIKOSI SUGU 

Chukua majani ya mti wa mbaazi  99 kisha yaandike majina ya Allah,kila jani moja na jina moja kisha yasomee  Suratul ALAMNASHRAHA mara 75 kisha yatwange kisha changanya na maji.

   Tumia kwa kuoga maji hayo na mengine tumia kwa kunywa kidogo.Inshaalla mikosi na nuksi sugu zitaondoka.utatumia kuandikia majina hayo kwa wino wa dhafarani.

  9.UKITAKA KUMUONA MTU MBAYA (MCHAWI)

 LIVE.

  Chukua majani ya mti wa mbaazi uliokomaa kisha changanya na majani ya kisamvu mpira kisha twanga pamoja,kisha kamua maji yake.maji hayo tumia kwa kunawia usoni 

,basi utawaona wachawi live.Na ukitaka kuondoa hali hiyo basi nawa kwa maji ya kawaida kwa nia ya kuondoa hali hiyo inshaallah.

  10.ANAYETAKA KUPENDWA AWE WAKIKE AU WA KIUME.

  Nenda katika mti wa mbaazi uliotoa maua kisha kikwangue magome yake yale ya juu kisha nenda kayaanike kisha uyasage kisha unga huo changanya na asali na maji ya mua kisha tumia maji hayo kwa kuoga kwa nia ya kuhitaji kupendwa au kukubalika katika jambo lolote ulitakalo.utaoga maji hayo kwa muda wa siku saba mfululizo kwa kutwa mara moja.

  11.KUMTIBU MTU ALIYECHANGANYIKIWA ;

Chukua majani ya mti wa mbaazi changanya na kitunguu swaumu,kisha twanga pamoja kisha mnyweshe mgonjwa huyo na majani mengine msugulie sehemu mbalimbali za mwili wake,inshaalla tatizo hilo litakuwa ni lenye kuondoka.utafanya hivyo kwa muda wa siku saba mfululizo asubuhi na jioni.

  12.KUMTIBU MTU ALIYEPOOZA;

  Chukua mzizi wa mti wa mbaazi  uchemshe umpe mgonjwa anywe ,pia chukua majani yake yaponde ponde kidogo kisha msugulie sehemu iliyopooza kwa nguvu kidogo.utafanya hivyo kwa muda wa wiki mbili au zaidi.

  13.KUJIKINGA DHIDI YA WASHIRIKINA NA UCHAWI:

  Chukua mzizi wa mti wa mbaazi kisha ukate vipande vidogovidogo saba kisha chemsha katika maji yasiyopungua lita moja.kisha utakunywa maji hayo  kwa nia ya kujikinga na shari za ushirikina na uchawi wao,hakika mwenyezimungu atakukinga na shari zao.

   Utakunywa maji hayo kikombe kidogo cha kahawa kimoja kwa muda wa siku saba mfululizo.

  14.KUFUNGA KESI AU MANENO KWENYE KIKAO.

  Chukua majani ya mti wa mbaazi na majani ya mti wa Dhambarau,kisha tafuna majani hayo huku ukitia nia yako juu ya kesi hiyo unalotaka liwe,kwa ajiri ya kufunga kesi hiyo au maneno katika kikao hicho.Inshaallah m/mungu atakutimizia .

   15.KURAHISISHA KUTOA KONDO LA MAMA LA UZAZI.

  Chukua majani ya mti wa mbaazi kisha yachemshe kisha mpe mama anywe kwa nia ya kuondoa kifungo kama amefungwa ili kondo la uzazi lisitike.Inshaallah m/mungu atamsaidia

 16.KUONDOA MAJI MENGI UKENI AU HARUFU MBAYA AU KUTOJISIKIA HAMU YA TENDO LA NDOA.

  Chukua majani ya mti wa mbaazi kisha yapondeponde majani hayo,kisha changanya na mafuta ya Alizeti au Zeituni kisha weka sehemu za siri valia na chupibau pedi ,pindi unapokwenda haja ndogo basi badilisha majani hayo kwa kuweka mengine.Unaweza ukatumia dawa hii kwa muda wa siku tatu mpaka saba mfululizo.

  INSHAALLAHU tatizo hilo litakwisha.

  17.KUTIBU KIFUA 

Chukua majani ya mti wa mbaazi tafuna majani hayo kisha meza maji yake.tumia  kwa muda wa siku tatu mfululizo asubuhi mchana na jioni kutafuna majani hayo inshaallah.

  18.KARUDISHA NYOTA ILIYOPOTEA AU KUSAFISHA NYOTA.

  Chukua mzizi wa mti wa mbaazi uliota kueleke upande wa mashariki(jua linakotokea)katakata vipande,kisha loweka katika maji kwa muda wa masaa24 kisha utatumia kuoga maji hayo kwa nia ya kusafisha nyota yako au kurudisha nyota yako.Tumia kuoga kwa muda wa siku saba mfululizo asubuhi na jioni.

 19.KUTOONEKANA NA MAADUI NA WATU WABAYA.

   Chukua mzizi wa mti wa mbaazi uanaolekea magharibi (jua linakozamia) twanga magome yake upate unga ,kisha unga huo changanya katika mafuta yako ya kupakaa kwa manuizi ya kutoonekana na watu wabaya.Au unaweza  kutumia kipande cha mzizi wa mti huo kama bakora au uweke kwenye wallet yako au mfuko wa suluali au sehemu yoyote kwa manuizi ya kujikinga usionekane na watu wabaya.

  Ukifanya hivyo hakika mtu yeyote atakaye kukusudia kwa ubaya hatoweza kukuona au kama ni mchawi hataweza kukuona kwa uwezo wa m/mungu.

   20.KUJITIBU UCHAWI WA KUKOSA PESA AU MAENDELEO.

  Chukua mzizi wa mti wa mbaazi  unaoelekea upande wa kaskazini,kisha utwange uanike ili upate unga wake.unga huo utatumia kwa kuchanganya kwenye maji ya kuoga au changanya kwenye mafuta ya Zeituni na utumie kwa kupakaa katika mwili wako na utajipakaa mafuta hayo asubuhi na jioni.

  21.KUMTIBU MWANAUME ALIYELOGWA KUTOSIMAMISHA SEHEMU ZAKE ZA SIRI.

   Chukua mzizi wa mti wa mbaazi unaoelekea chini (mzizi mkuu) bandua magome yake,kisha chemsha katika maji ya kutosha.Mpe mgonjwa anywe kikombe kimoja asubuhi mchana na jioni,atatumia dawa hiyo kwa muda wa siku tatu mfululizo.usisahau kutia nia ya kuondosha tatizo hilo pindi unakunywa dawa hiyo.

    22.KUTIBU HEDHI ISIYOKOMA AU FISTURA (MWANAMKE KUKOJOA MARA KWA MARA BAADA YA KUJIFUNGUA)

   Chukua mzizi unaoelekea chini bandua magome yake kisha chemsha katika maji yakutosha kisha kunywa dawa hiyo kwa nia ya kuondosha tatizo hilo.Inshaallaha utakunywa kikombe kimoja cha chai asubuhi, mchana na jioni utafanya hivyo kwa muda wa siku tatu hadi saba mfululizo.kwa uwezo wa m/mungu tatizo litakuondoka.

   23.KUMGANDISHA MCHAWI ENEO LAKO.

    Chukua kijiti  cha mti wa mbaazi,kisha toboa tundu katikati katika kijiti hicho ,kisha tia ndani yake mbegu tatu(3) za Lufyambo kisha ziba na nta katika tundu hilo.Fimbo hiyo iweke juu ya mlango wako wa nyumba.sehemu hiyo mchawi yeyote atakayekuja eneo hilo kichawi au kwa nia ya kufanya uchawi basi ataganda na hataweza kutoka katika eneo hilo.

    JINSI YA KUMZINDUA.

**Unaweza kumsemesha kwa kumkusudia atoke katika hali ile kisha ukamruhusu aondoke eneo hilo.

     AU

Kama utahitaji kumuangamiza au kumtia madhara basi chukua ile fimbo yako ya mti wa mbaazi kisha mpige nayo fimbo moja kisha mwambie aende zake au chukua fimbo iliyotokana na mti wa muhogo umpige nayo mara moja tu kisha mwambie aondoke.hakika hataweza kuishi zaidi ya siku 21 atakufa kwa uwezo wa m/mungu na jambo hili ni hatari sana.

   24.KUTIBU SEHEMU ZA SIRI ZA MWANAUME ZILIZOSIMAMA WIMA BILA KULALA.

   Chukua majani ya mti wa mbaazi kisha changanya na mzizi mkuu (mzizi unaolekea chini katika mti wa mbaazi) kisha chemsha vyote pamoja kisha mpe mgonjwa anywe  kutwa mara tatu kikombe kimoja cha  chai.Atafanya hivyo kwa muda wa siku tatu mfululizo inshaallah tatizo litakwisha.

   25.KUMCHARAZA MCHAWI BAKORA.

Chukua mzizi wa mti wa mbaazi wowote kisha ukate vipande vidogovidogo vinne kisha tafuta matunda manne ya ndulele/mturatura kisha funga pamoja kipande kimoja cha mzizi wa mbaazi na tunda moja la mturatura kisha weka katika kila pembe ya nyumba yako au chumba chako.unaweza kufukia chini au  ukaweka juu.Eneo hilo endapo mchawi atakuja kuchezea katika mazingira ya kichawi basi atapigwa bakora mpaka atakapoondoka eneo hilo.Usisahau kuweka nia yako pindi unapofanya jambo hilo.

   26.KUTIBU MAUMIVU MAKARI YA SIHIRI (UCHAWI).

 Chukua majani ya mti wa mbaazi kisha yachemshe,wakati wa kunywa tia nia ya kuyaondosha hayo maumivu yalio katika mwili.utakunywa kikombe kimoja asubuhi,mchana na jioni kwa muda wa siku tatu mfululizo.

   Inshaallah maumivu hayo yatakwisha.

   27.KUPOTEA KWA PESA NDANI YA NYUMBA KWA KUTATANISHA.

 Chukua mzizi wa mbaazi wowote kisha utwange upate unga wake,unga huo changanya kwenye maji kisha pigia deki ndani ya nyumba yako yote.Inshaallah uadui wa kupotea pesa utakwisha.

  28.UKITAKA WACHAWI WASIKUONE.

Chukua kijiti cha mti wa mbaazi kitoboe katikati kisha andika aya ya 9 ya suratul YASIIN kwa karamu  nyeusi katika karatasi kisha kipachike katiks tobo hilo alafu kisomee aya ya hiyo ya 9 mara 90.

   Inshaallah watu wabaya hawatakuona pindi utakapo tembea na kijiti au fimbo hiyo njiani au mahari popote.

   29.UKITAKA KUONA CHOCHOTE KATIKA USINGIZI.

Chukua mzizi wa mti wa mbaazi ukate kipande kidogo kisha utoboe tundu kisha chukuwa unywele wa katikati ya kichwa chako ung'oe kisha weka katika tobo hili.kisha ziba na nta au kitu chochote.wakati wa kulala chukua hicho kipande cha mzizi kisha nuia kile unachotaka kukiota kisha weke hicho kipande cha mzizi sehemu ambayo unachegemea,utaona kile ulichokikusudia inshaallah.

   30.KUVUTA WATEJA KATIKA BISHARA YAKO.

  Chukua mzizi wa mti wa mbaazi utwange upate unga wake kisha,kisha weka kwenye maji weka na chumvi ya mawe kidogo .kisha weka na yai la kuku wa kienyeji likiwa zima.kisha yasomee hayo maji suratul WAQIAAH mara 16 kwa nia ya kuvuta wateja katika biashara yako.

   Tumia maji hayo kwa kupigua deki katika eneo la biashara yako au mwagia mwagia eneo la biashara yako asubuhi au jioni.Inshaallah utaona maajabu yake.

30. KUVUNJA AINA MBALIMBALI ZA UCHAWI KATIKA MWILI.

   Chukua majani ya mti wa mbaazi,kisha yachemshe tumia kwa kuoga huku ukiwa umetia nia ya kuvunja uchawi  katika mwili wako.Utatumia dawa hiyo kwa muda wa siku saba mfululizo.

31. KUMCHAPA BAKORA MCHAWI.

 Chukua majani ya mti wa mbaazi na majani ya mti wa parachichi changanya na chumvi ya mawe kiasi cha gao la mkono mmoja kisha twanga pamoja, kisha anika kwenye jua mchanganyiko huo.Baada ya kukauka funga kwenye kitambaa mchanganyiko huo kisha weka sehemu unayotaka kama ni chumbani au sehemu yeyote ulioikusudia,basi eneo hilo mchawi yeyote akija eneo hilo kichawi basi atachapwa bakora mpaka atakapoondoka eneo hilo.

 32.KUPUNGUZA IDADI YA SIKU ZA HEDHI KWA MWANAMKE.

 Nenda katika mti wa mbaazi kisha chuma majani matatu pande nne za mti huo,kisha chemsha majani hayo  na baada ya kuchemsha tia nia yako kwamba unataka kupunga idadi ya siku za kutumika ukiwa mwezini.kisha utakunywa dawa hiyo kwa idadi ya siku unazotaka utumike mfano siku tatu basi utakunywa siku tatu dawa hiyo na kama ni siku nne basi utakunywa siku nne dawa hiyo.Na katika kunywa utakunywa kikombe kimoja kutwa mara moja tu.

  Inshaallah siku za kutumika zitakuwa ni zenye kupungua kwa uwezo wa m/mungu.

33.KUMVUTA MUME/MKE /MPENZI AU NDUGU ALIYOKO MBALI;

  Chukua majani ya mti wabaazi yaliyonyauka changanya na baruti na mti uliopigwa na Radi kisha choma kwa nia ya kumuita muhusika unayemuhitaji.

  Choma kwa muda wa siku tatu mpaka saba inshaallah mtu huyo atakuwa ni mwenye kuja kwako.

34.KINGA YA KUWAZUIA WACHAWI WASIINGIE NDANI YA NYUMBA YAKO.

   Chukua mzizi wa mti wa mbaazi na mzizi wa mti wa mbalika(nyonyo) kisha funga pigi nne kwa kuchanganya mizizi yote miwili pamoja.funga pigi hizo kwa kitambaa cheusi ,kisha zisomee pigi hizo Ayatil Qursiyyu mara 170 kwa nia ya kutaka mwenyezi mungu akupe kinga katika eneo lako.kisha ziweke pigi hizo katika pembe nne za nyumba yako au chumba chako.Inshaallah hata waje wachawi 1000 hawawezi kuingia ndani ya nyumba yako na kukufanyia ubaya.

  35.KUMPIGA BAKORA MCHAWI.

Chukua fimbo ya mti wa mbaazi kisha itoboe tundu katikati kisha weka unga wa kinyonga ndani ya tundu hilo alafu ziba kwa nta au kitu chochote.Fimbo hiyo ukiiweka sehemu ya mlango wako  akija mchawi eneo hilo atapigwa bakora mpaka atakapo ondoka eneo hilo.

  Na kama fimbo hiyo utatembea nayo wachawi watakuogopa sana na kukupa heshima kubwa sana.

  36.KUFUKUZA MAJINI WABAYA KATIKA MWILI.

   Chukua majani ya mti wa mbaazi,miatusaili,Ndulele 11 na uzikate vipande viwiliviwili,Ndimu saba nazo uzikate vipande,kivumbasi na mvuje/Halititi kisha changanya na maji chemsha kisha jivukize au mvukize mgonjwa.utafanya hivyo kutwa mara moja kwa muda wa siku tatu hadi saba mfululizo inshaallah majini hayo yataondoka kwa uwezo wa mwenyezimungu.

   mpaka hapa nimejitahitid kuelezea matumizi mbalimbali ya mti huu wa mbaazi,lakini mti huu unamatumizi mengi sana zaidi ya hayo niliyoyaeleza.Nakusihi tu usikose kutembelea mitandao yangu ya kijamii kwa ajiri ya kujifunza elimu ya tiba kupitia mitishamba,matunda na dua kupitia kitabu kitukufu cha Quran kwa kobofya link zilizopo hapo chini.

   Unaweza kuniachia Coment yako hapo  chini nami takufatilia inshaallah.



  

Previous Post Next Post

Contact Form