MAGONJWA YASIYOTIBIKA HOSPITALINI.

FAHAMU JINSI YA KUJITIBU MAGONJWA YASIYOTIBIKA HOSPITALI.

  Mwenyezimungu amemuumba mwanadamu,na huyo mwanadamu maishani mwake ataishi kwa kupitia misukosuko mbalimbali au mitihani mbalimbali ikiwemo maradhi na mitihani mingine.

   Hata hivyo anapopatwa na maradhi asikae tu hivi hivi bila ya kujitibu,ni lazima kwake kufuatilia kwake matibabuili apone.Kwani ugonjwa wowote ule ni lazima uwe na dawa yake.Haiyumkiniki mwenyezimungu alete ugonjwa alafu ukose dawa.miongoni mwa baadhi ya wengi wetu wamezoea kujitibu hospitalini na wanapona kwa asilimia kubwa tu.Lakini kuna wengine  hupatwa na maradhi na wakafanyiwa uchunguzi wa kina kupitia vipimo mbalimbali vya kimaabara  na ugonjwa ukakosa kuonekana pamoja na kwamba huyo mgonjwa atalalamika maumivu makali sana.

  Mara nyingi hatua inayofuata ni kumtoa mgonjwa hospitali na kumpeleka kwa waganga wa kienyeji ambao asilimia kubwa miongoni mwao hutibu kwa njia za kishirikina ambazo hata kama mgonjwa atapona bado kesi ya kumkufuru mwenyezimungu itabaki palepale na adhabu itathibiti juu ya mgonjwa na wauguzi wake juu ya jambo hilo mbele ya m/mungu.

   Yapo maradhi ambayo huwa yanasa babishwa na mashetani  wa kijini  pindi wamuingiapo mtu kwa lengo la kumtesa ili ashindwe kuhimili maumivu ili afanye tiba za kishirikina na waende nae motoni.Au jini humuingia mtu kwa vile huyo mtu amerogwa na jini ndiye anaemsumbua kiwiliwili,au jini amemuingia mtu kwa kumfanyia ujeuri kama kumuangukia  au kumkanyaga na mambo mengieyo,naye akaamua kulipiza kisasi kwa huyo  mtu aliye mtendea hayo endapo mtu huyo anaishi bila  ya kufuata taratibu za kujikinga na shari mbalimbali ikiwemo na hiyo ya jini kwa kufuata taratibu za kujikinga na shari malimbali ikiwemo na hiyo ya jini  kwa kufuata mafundisho ya mtume (s.a.w)basi huyo jini itakuwa siyo kazi ngumu kwake kumuingia na kumtaabisha

   Jambo lingine ni kwamba jini anaweza kumsumbua mwanadamu  kwa kumletea maradhi mbalimbali ambayo nayo hayatotibika hospitalini  kwa vile tu anazini nae  usingizini  na anamfanyia  chuki endapo huyo mtu  anafanya tendo hilo na binadamu mwenzake akiwa mume kwa mke wake na akiwa mke kwa mume wake,hapo yeye hushikwa na wivu na huanza kumletea mateso kwa vile amemtawala ndani ya kiwiliwili chake.Hawa wote  inabidi wapate tiba kwa ville hospitalini watashindwa kutibiwa itabidi wafanyiwe  matibabu ya kusomewa Ruqya ya sheria inshaallah watapona

        (Isra :82)

        UFUMBUZI WA MAGONJWA                        YASIYOTIBIKA HOSPITALI.

Pamoja na kuelezea baadhi ya magonjwa yasiyotibika hospitalini na athari ya kutibiwa kishirikina bado yapo maradhi ambayo hayatibiki hospitalini na vilevile washirikina hawawezi kuyatibu.

  Mara nyingi maradhi haya husababishwa na jini aliyemuingia mwanadamu kwa njia ya uchawi nae lengo lake ni kumsumbua huyo mwanadamu  mpaka afe kwa mujibu wa maelekezo aliopewa na wakubwa zake wa kijini na akikiuka huadhibiwa.

   Kwa maana hizo tiba zinazofanywa kwa wagonjwa wanamna hiyo ni kafara za kishirikina yaani zawadi kwa yule jini kwa namna ya kumrubuni kama vile namna ya rushwa ili akiuke maagizo ya wakubwa zake na aache kumsumbua yule mtu.Hii ndio maana ya kafara ya kishirikina ambayo ni lazima ziwepo zawadi kama kuku,nazi,mbuzi,n.k kwa ajiri ya hao majini.Kinacholeta tabu hapo ni kwamba huyo jini anayemsumbua huyo mgonjwa huenda amepewa zawadi kubwa sana ili kuifanya kazi hiyo,au ameahidiwa zawadi kubwa mfano amechinjiwa ng'ombe au mbuzi au ameahidiwa vitu hivyo endapo atamaliza hiyo kazi aliyotumwa nawe unamfanyia kafara ya kuku au njiwa yeye hawezi kukubali kuvunja agizo la bwana wake kwa hiyo hongo ndogo ndogo tu.

   Ndio maana baadhi ya watu huandaliwa hizo kafara na wakapandisha shetani wa kijini na asile hivyo vitu kwa vile huona siyo kitu cha maana kwake kwa vile anapewa ama ameahidiwa zaidi ya vitu hivyo.Wengine hupandisha mashetani nyumbani tu na wakishafanyiwa taratibu za hizo tiba za kupeana zawadi basi huko kwa waganga  hawapandishi na kama wakipandisha basi hukataa kula hizo zawadi.

     Shetani yeyote anapomwingia mtu na kumtesa,kiongozi wake  humuwekea ulinzi ili asikiuke maadili ya hiyo kazi ndipo humfatilia popote aendapo ili kumzuia asikubali kupokea rushwa kwa hao waganga wa kishirikina pindi wafanyapo matibabu yao.

   Ndio maana kuna wakati mtu afanyiwapo Ruqya(kisomo cha Quran) ya sheria hupanda shetani na akashindwa kuondoka kwa vile amezuiwa na wenzake pamoja  na kwamba mwenyewe atakuwa yu radhi kuondoka lakini hushindwa kwa huko kutenzwa nguvu na hao wanaomlinda ili asitoke,hiyo ndiyo sababu inayomfanya mtu asipone hata aumwe maradhi yanayotibika kishirikina.Hata hivyo katika tiba za ruqya(visomo vya Quran) hilo sio tatizo hata azingirwe vipi yapo mambo ambayo huelekezwa na akaweza kuondoka bila ya kumdhuru hao walinzi.


 

  

Previous Post Next Post

Contact Form