FAIDA ZA MMEA WA ALOVERA KATIKA TIBA.


 
   Mmea wa Alovera ni miongoni mwa mimea yenye faida nyingi sana katika kutibu maradhi mbalimbali yanayoweza kumsibu binadamu.

  Miongo mwa maradhi yanayoweza kutibika kupitia mmea huu ni pamoja na maradhi yafuatayo;

1.KUONDOA SUMU MWILINI.
  Kama unahitaji kuondoa sumu mwilini utachukua jani la alovera  kisha utalikata kata vipande vidogo vidogo kisha utachukua na tangawizi nayo utaikatakata vipande vidogo vidogo  kisha utachemsha pamoja katika maji  kwa muda dakika 20 kisha baada ya hapo utaipua dawa yako na kuacha ipoe.Kisha utaichuja halafu utakwenda kuiweka kwenye friji au sehemu yenye ubalidi sana  ikae masaa 12 kisha baada ya hapo utatumia dawa hiyo kwa kunywa grasi moja kutwa mara mbili kwa muda wa siku saba.

  2.KUTIBU MARADHI YA NGOZI(mfano,upele)
  Kama unahitaji kutibu maradhi ya upele   katika mwili hapa kuna njia mbili za kutibu maradhi hayo.
  **1.Utachukua jani la Alovera kisha  utalikata juu nchani kisha utachukua ule utomvu wake kisha utatumia kupakaa katika ngozi  sehemu yenye maradhi hayo utafanya hivyo asubuhi na jioni ndani ya siku saba au zaidi.

  **2.Utachukua majani ya mualovera kisha utayaanika katika jua mpaka yakauke kisha utayasaga upate unga wake,kisha unga huo utatumia kuchanganya katika mafuta ya nazi kisha utakuwa unajipakaa mafuta hayo sehemu yenye maradhi ya ngozi. Utafanya hivyo asubuhi na jioni .

3.KUTIBU KIDONDA  CHA MUDA MREFU KATIKA MWILI.
  Utachukua jani la alovera kisha utalianika katika jua mpaka likauke kisha utalisaga upate unga wake,kisha unga huo utatumia kuweka kwenye kidonda,Utafanya hivyo asubuhi na jioni kwa muda wa siku saba hadi 14 inshaallah utakwenda kupona tatizo hilo.

4.KUTIBU TATIZO LA SUKARI SUGU.
  Kama unasumbuliwa na tatizo la sukari sugu  utachukua jani la alovera  kisha utalimenya yale maganda yake ya juu kisha utalisaga katika brenda  upate ile juisi yake kisha juisi ile utachanganya na juisi ya ndimu au limao.Kisha utatumia juisi hiyo kwa kunywa asubuhi na jioni kwa muda wa siku  14 inshaallah utakuwa vizuri.

5.KITIBU TATIZO LA KUKOSA HAMU YA TENDO LA NDOA.

   Utachukua jani la Alovera  kisha utalikata kata vipande vidogo vidogo ,kisha utalitia katika sufuria  la maji  kisha ndani yake  utaweka na unga wa mdalasini  kisha utachemsha  katika jiko la moto.Baada ya dawa yako kuchemka vizuri utatumia  kwa kunywa grasi moja  asubuhi na jioni kwa siku saba zenye kufuatana. Inshaallah utakwenda kuondokana na changamoto hiyo.

6.KUONGEZA KINGA MWILI (CD4) KWA HARAKA.
  Kama unahitaji kuongeza kinga mwili kwa haraka basi  utachukua jani la muoalovera kisha utalikatakata  vipande vidogo vidogo kisha  utaliweka ndani ya maji likae masaa 12 ndani yake .Baada ya hapo utachuja  maji hayo vizuri kisha utatumia maji hayo kwa kunywa  grasi moja asubuhi na jioni fanya hivyo kwa siku saba mfululizo.

7.KUTIBU MARADHI YA KUKU NA KUWAPA KINGA YA MWILI.
   Kuna njia mbili za kutibu maradhi haya ya kuku kupitia mmea huu,
1.Utachukua jani la mualovera  kisha utalikata vipande vidogo vidogo  kisha itaweka katika maji ya kuku ya kunywa.
  2.Utalikausha jani la  alovera  kisha  baada ya kukauka vizuri utalisaga upate unga wake.Unga huo utatumia  kuchanganya katika chakula cha kuku mfano pumba n.k

8.KUDHIBITI MARADHI YA SALATANI.
   Kama unahitaji kudhibiti maradhi ya saratani katika mwili basi utatengeneza juisi itokanayo na majani ya Alovera kisha ndani yake utachanganya na maji ya tangawizi,kisha utatumia juisi hiyo kwa kunywa  grasi moja asubuhi na moja jioni.Fanya hivyo kwa muda wa siku  saba mpaka 14.

9.KUTIBU PRESHA YA KUPANDA.
  Kama unahitaji kutibu presha ya kupanda basi utachukua jani la Alovera kisha  utalikata vipande vidogo vidogo kisha utatia katika maji alafu utaacha kwa muda wa masaa mawili,baada ya hapo utachuja vizuri maji hayo kisha  utatumia kwa kunywa grasi moja asubuhi na gras moja jioni.

10.KITULIZA  KIUNGULIA
  Kama umepata changamoto ya kupata kiungulia  baada kula chakula basi utatumia  jani la mualovera kisha utalikatakata vipande vidogo vidogo  kisha utatia katika  grasi ya maji kisha utaacha kwa muda wa dakik 5 alafu utatumia maji hayo kwa kunywa  kidogo kidogo inshaallah kiungulia kitakwisha.

11.KUTATUA TATIZO LA KUPATA CHOO KWA SHIDA.
Kama unasumbuliwa na tatizo la kupata  choo kwa shida ,basi tengeneza juisi itokanayo na jani la Alovera,kisha changanya na unga wa  tangawizi  nusu kijiko  katika grasi moja ya juisi hiyo,kisha tumia kunywa nusu grasi asubuhi na jioni.
  Fanya hivyo kwa muda wa siku tatu mfululizo inshaallah utapata choo.

  12.KUTIBU TATIZO LA FANGASI.
  Kama unasumbuliwa na tatizo la fangasi sehemu yoyote katika mwili wako,utachukua jani la Alovera kisha utalipasha kidogo katika jiko la moto alafu utatumia kusugulia sehemu zenye fangasi kwa muda wa dakika mbili mpaka tatu.Utafanya hivyo asubuhi na jioni. Fanya hivyo mpaka pale utakapopata nafuu ya kutosha.

  13. KUTIBU TATIZO LA VIDONDA VYA TUMBO.
   Kwa ajiri ya kutibu vidonda vya tumbo utatengeza juisi itokanayo na jani la Alovera kisha utatia ndani yake  na vijiko viwili vya asali katika grasi moja kisha utatumia kunywa grasi moja kutwa mara tatu.
Fanya hivyo kwa muda wa siku 30 hadi 45 inshaallah utaondokana na changamoto hiyo.

14. KUTIBU TATIZO LA MINYOO TUMBONI.
  Kama unasumbuliwa na tatizo la minyoo tumboni basi tumia juisi iliotokana na jani la mualovera na ndani yake pia unaweza kuchanganya na nusu kijiko cha unga wa mbegu za papai kisha tumia kunywa  nusu grasi kutwa mara tatu.Fanya hivyo kwa muda wa siku tatu hadi saba inshaallah utakuwa vizuri.

15.KUTIBU TATIZO LA KUPASUKA KWA VICHWA VYA WATOTO WADOGO.
   Kama mtoto wako anashida ya kupasuka kwa kichwa chake baada ya kuzaliwa basi utatumia jani la muolovera kulipasha kidogo katika jiko la moto kisha tumia kumkandia kandia sehemu hiyo inayopasuka kichwani.Fanya hivyo asubuhi na jioni kwa muda wa wiki moja mpaka mbili, inshaallah ataondokana na changamoto hiyo.

Hizi ni baadhi ya faida zipatikanazo kupitia mmea huu wa alovela,lakini zipo faida nyingi sana tunazoweza kuzipata kupitia mmea huu wa Alovera katika kutibu maradhi mbalimbali.


Unaweza kupata masomo mbalimbali yanayohusu elimu ya mitashamba kwa kutembelea  katika mitandao yangu ya kijamii kama ifuatavyo;

Facebook-Tiba facts na

         Qur'an and Herbals medicine


Instagram-ustadh.bashir/@tibafacts


Youtube-tibafacts online tv


Utapata mafunzo mbalimbali yatakayokusaidia kuhusu elimu ya tiba kupitia mitishamba na matunda.


Previous Post Next Post

Contact Form