FAIDA ZA MTI WA KIFA UONGO/SHUNTAMA

 MTI WA KIFA UONGO;

Huu ni mti wenye maajabu makubwa katika ulimwengu wa tiba.Umeitwa mti wa kifa uongo kutokana na tabia yake ya kujirinda pindi unaposogelewa na hasa unapoguswa na adui,mti huu huwa unajikunja na kuyafanya majani yake kuonekana kama yamekauka na kusinyaa,na pindi adui anapoondoka mti huu hurejea katika hali yake ya kawaida.Wengine huuita mti wa hisia kutokana na tabia yake ya kusinyaa kwa majani yake pindi unapohisi kuwa umeshikwa na adui.

   Sasa katika ulimwengu wa tiba mti huu unasiri nyingi sana na unauwezo wa kufanya maajabu mengi katika matatizo mbalimbali ikiwemo katika kumuadhibu adui au mtu mbaya anayekuja kukuchezea katika eneo lako,pia ni mvuto mkali katika mapenzi biashara na shughuri mbalimbali,pia una uwezo wa kufufua mapenzi yaliyokufa au kupungua baina ya wanandoa,ni limbwata kali sana la mapenzi na lenye uwezo wa kumuinamisha mme au mke na akawa ni mwenye kukutii katika yote unayoyahitaji.Pia mti huu hutibu sukari,Presha,na tumbo kujaa gesi.

   Sasa twende takaangalie baadhi ya faida za mti huu kwa ufafanuzi zaidi.

1.LIMBWATA KALI SANA LA MAPENZI.

   >>Nenda katika mti wa kifa uongo majira ya asubuhi kuanzia majira ya saa moja hadi saa tano,ukiwa na udi au nafaka yoyote mfano ulezi,mtama au ufuta kidogo.Kisha ukifika katika mti huo washa udi wako,au mwaga zile nafaka zako kisha tia nia yako ya kumuomba mwenyezimungu kwa baraka na utufu alizoupa mti huu muombe unahitaji kuuchukua  ili ukakufanyie vile unavyohitaji katika mapenzi yako.Na sababu za kwenda na vitu hivyo mti huu una maruhani na malaika wanaoutumikia mti huu kwaiyo kumwaga zile nafaka zako pale au kuchoma udi hiyo ni kama kutoa sadaka na kuhitaji ukubaliwe katika yale mambo yako.

   Kisha chimba mzizi wa mti huo unaoelekea upande wa mashariki (upande ambao jua linachomozea),kisha nenda ukausage au kuutwanga ili upate unga wake.

 Unga huo  utauchanganya na asali kidogo kisha utapakaa sehemu zako za siri kidogo pindi unapotaka kumuingilia mkeo au kuingiliwa na mumeo kisha nuia vile unavyotaka iwe,kwa kutumia kidole cha kati katika mkono wowote kisha utamuingilia mkeo au utaingiliwa na mumeo na pinda mnaposhiriki tendo hilo utakuwa unakusudia kimoyomoyo yale unayoyataka mpaka utakapomaliza.

    NB:

 Limbwata hili ni hatari na ni kali sana hivyo usimfanyie mtu ambaye huna malengo naye ya kukaa naye mda mrefu au kumuoa,pia sio la kufanyia majaribio kwa mtu ambaye humpendi atakuganda mpaka utaona kero.

   2.KUTIBU TATIZO LA KUKOSA HISIA ZA MAPENZI KWA NJIA ZA VIFUNGO VYA KICHAWI.

  >> Nenda katika mti huo kisha chukua majani ya mti huo ya kutosha kisha nenda nayo nyumbani,changanya na tangawizi mbichi kisha chemsha pamoja katika maji.Tumia kwa kunywa dawa hiyo kikombe kimoja asubuhi na jioni kwa muda wa siku saba huku ukiwa unatia nia yako ya kuondoa tatizo hilo.Inshaalla tatizo litakwisha.

  3.KUFUFUA AU KUNAWIRISHA MAPENZI YALIOKUFA BAINA YA WANANDOA.

 >>Nenda katika mti wa kifaungo kisha ukifika katika mti huo linuilie jani moja kabla ya kuligusa na kulichuma nia yako ya kumuomba m/mungu unahitaji kulichukua jani hilo ili likakusaidie kufufua au kunawirisha mapenzi yako kisha lichume jani hilo kabla hujaligusa nenda nalo nyumbani kisha lianike alafu ulisage upate unga wake.Unga huo utumie kwa kuchanganya kwenye mafuta ya kupakaa ambayo mtakuwa mnapakaa nyinyi wote wawili.Utaona maajabu ya dawa hiyo,hakika mtapendana sana nyinyi nyote pamoja.

     4.MVUTO MKALI KATIKA MWILI,MAPENZI,NA SEHEMU MBALIMBALI PIA KUONDOA NUKSI NA MIKOSI SUGU.

  >>Chukua majani ya mti wa kifa uongo,maua yake,na mizizi zake kisha itwange pamoja mpaka upate unga wake.

   Unga huo utautumia kwa kuchanganya kidogo katika maji yako ya kuoga,kisha utakoga kwa manuizi yale uyatakayo kama ilivyoelezwa hapo juu.koga kwa muda wa siku saba asubuhi na jioni,pia unaweza kuchanganya na mafuta yako ya kupakaa ukawa unapakaa asubuhi na jioni kwa manuizi unayotaka inshaallah.

    5.PIGO LA KUMUADHIBU MCHAWI ANAYEKUSUMBUA NDANI YA NYUMBA YAKO.

    >>Nenda katika mti wa kifa uongo pindi jua linapoelekea kuzama kisha nuia juu ya matatizo yako unayoyakusudia ya kutaka kumuadhibu mchawi anayekusumbua katika nyumba yako kisha chuma matawi saba ya mti  wa kifa uongo kisha utakapofika nyumbani majani hayo utayalaza nje katika jiko la kuni lisilo na moto kisha asubuhi yaweke ndani yalale katika nyumba kwa muda wa siku saba.Kisha siku ya nane chukua majani hayo kisha yachome katika jiko la  mkaa kwa manuizi ya kutaka mtu anayekuja kukufanyia ubaya basi awe ni mwenye kupata adhabu kari na chungu kupitia uwezo alioupa mwenyezimungu mti huo inshaallah kama atakuja mtu mbaya katika nyumba yako basi utamsikia anakohokoho na ataondoka eneo hilo akiwa yuko hoi kabisa kutokana na dawa hiyo inshaallah.

  6.KUTIBU SUKARI,PRESHA NA TUMBO KUJAA GESI.

   >>Chukua majani ya kifauongo yaanike kisha yasage upate unga wake kisha tafuta na majani ya mchunga au mgagani (hii ni mboga chungu  nayo ianike uisage nayo upate unga wake,)kisha mchanganyiko huo utaweka kijiko kimoja katika kikombe cha maji ya vuguvugu au kikombe cha uji kisha utatumia kwa kunywa asubuhi na jioni gras moja utatumia dawa hiyo kwa muda wa wiki mbili hadi tatu inshaallah tatizo hilo litakua ni lenye kuisha.


     Unaweza kutembelea mitandao yangu ya kijamii kwa ajiri ya kujifunza tiba mbalimbali kupitia Dua mbalimbali,mitishamba na matunda.

Facebook-Tiba facts

Youtube-tibafacts online tv

Instagramu-Ustadh.bashir/@tibafacts


Pia unaweza kujipatia vitabu vyangu vinavyofundisha Elimu ya tiba ukiwa nchi yoyote dunia tunakutumia kwa njia ya mtandao.

1.MAAJABU YA MITISHAMBA KATIKA KUTIBU MARADHI YA KIJINI NA UCHAWI, No.1

Kwa shilingi 7000/= za kitanzania


2.MAAJABU YA MITISHAMBA KATIKA KUTIBU MARADHI YA KIJINI NA UCHAWI,No.2

Kwa shilingi 10000/=


3.TIBA MBADALA KWA MAGINJWA YA KIBAIOLOJIA.

Kwa shilingi 10000/=

4.MAAJABU YA QUR'AN KATIKA KUTIBU MARADHI NA KUONDOSHA SHIDA MBALIMBALI.

Kwa shilingi 12000/=

5.UTUKUFU WA MAJINA 28 YA BARHATIH NA KAZI ZAKE.

Kwa shilingi 15000/=


vitabu vyote unaweza kutumiwa kwa njia ya mtandao ukiwa nchi yoyote duniani.


Wasiliana nami kwa 

Sim.+255757455646

au

+255672410104


Namba zote zinapatikana whatsApp

    


Previous Post Next Post

Contact Form