TIBA KUPITIA MITISHAMBA NA MATUNDA:
MTI WA MUEMBE.
Mti wa muembe ni miongoni mwa miti yenye maajabu na matumizi mengi katika ulimwengu wa tiba za mitishamba na matunda.Mti wa muembe unaweza ukatumika kutibu maradhi aina mbalimbali ikiwemo maradhi ya kawaida na maradhi yatokanayo na ushirikina.Mti huu ni miongoni mwa miti inayopendwa sana na watu wabaya hasa washirikina na ndio sehemu washirikina wanapenda kuweka kituo chao wanapokuwa katika shughuri zao za kichawi.pia katika mti wa muembe ndio sehemu ambapo wanapoweza kuwapumzisha misukule (watu waliokufa) pindi wanapotoka katika shughuri zao hasa za shambani.Kwaiyo sio vizuri mtu kupenda kupumzika au kulala chini ya mti wa muembe hasa iliyoko nje ya mji au inayopatikana mashambani.
Sasa tuangalie faida za mti wa muembe kati ulimwengu wa tiba kupitia mitishamba na matunda.
1.KUTIBU TATIZO LA KUKOSA HAMU YA TENDO LA NDOA.
>>>Chukua maua ya mti wa muembe kisha yakaushe kisha yasage uchanganye na uji wa mtama au ulezi .Kunywa kikombe kimoja au viwili asubuhi na jioni Inshaallah tatizo litakwisha kabisa.
2.KUTIBU TATIZO LA KIBAMIA (UUME KUWA MDIGO)
>>>Chukua kokwa la embe lisage upate unga wake kisha unga huo changanya na mafuta ya ngo'ombe mabichi (SAMRI) kisha utachukua maji ya vuguvugu kidogo utakandiakandia sehemu za siri kidogokidogo kwa muada wa dakika tano,kisha utapaka dawa yako hiyo na kuanza kuuchua uume huo ukianzia kwenye shina la uume kuelekea kwenye kichwa.
Utafanya hivyo asubuhi na jioni kwa muda wa wiki mbili mfululizo inshaalla utapata matokeo unayoyahitaji.
3.ALIE FUNGWA ASIPATE MIMBA.
>>>Chukua majani ya mti wa mbaazi na magome ya mti wa muembe kisha yaloweke kisha kwa muda wa masaa 3 kisha tumia kwa kunywa kwa muda wa siku 7 au zaidi pia utatia nia yako ya kuondisha tatizo hilo la kufungwa ili usioate ujauzito pindi unapokunywa dawa hiyo.
4.KUUWA UCHAWI KATIKA ENEO LAKO.
>>>Chukua jivu la mti wowote,chumvi ya mawe na majani ya muembe yaponde kisha changanya vyote hivyo kisha tumia kwa kuoga au kupigia deki eneo hilo.
5.KUPATA MVUTO WA AJABU KAZINI AU KATIKA JAMII.
>>>Tafuta aina sabaza miembe,kisha chukua majani yake.Yapondeponde majani hayo kisha tumia kwa kuoga utaona maajabu ya dawa hiyo katika mvuto.
AU
Unaweza kuyakausha majani hayo kisha ukatumia kwa kuchoma katika jiko la mkaa kama utahitaji kumvuta mtu aliekukimbia mfano mume,mke, mpenzi au ndugu nawe unahitaji aludi kwako.
Tukiwa tunaendelea kuuelezea mti wa muembe leo tena tuangalie baadhi ya faida za mti huo na magonjwa unayoweza kujitibu kutokana na mti huo.
6. KUVUNJA UCHAWI KATIKA MWILI.
>>>Chukua majani ya muembe kisha chemsha alafu koga maji hayo kwa manuizi ya kuuwa uchawi uliokatika mwili,utafanya hivyo kwa muda wa siku tatu asubuhi na jioni.
Inshaallah uchawi utakuwa umebatilika.
7. KUMTIBU MTU MWENYE KICHAA.
>>>Chukua magome ya ndani ya muembe pande nne katika mti huo,kisha yafunge pamoja kisha yachemshe alafu mpe mgonjwa atumie kwa kunywa.atumie dawa hiyo kwa muda wa wiki moja.inshaallah tatizo litakwisha.
8.KUTIBU UGONJWA WA KISUKARI.
>>>Chukua majani machanga ya mti wa muembe kisha chemsha alafu yatumike kwa kunywa maji hayo kikombe kimoja cha chai kutwa mara tatu .Atatumia dawa hiyo kwa muda wa wiki mbili au zaidi mpaka pale atakapo ona tatizo limekwisha kabisa.
9.KUTIBU TATIZO LA KWIKWI.
Chukua majani ya mti wa muembe kisha yachemshe alafu jivukize,(kupiga nyungu) ni tiba nzuri ya tatizo la kwikwi ya muda mrefu.
10.KUTIBU TATIZO LA KUHARISHA DAMU.
>>>Chukua magome ya muembe yale ya ndani kwangua kisha chemsha alafu mpe mgonjwa anaye harisha damu kikombe kimoja cha chai kutwa mara tatu kwa muda wa siku tatu hadi saba.
11.KUTIBU MENO YANAYOTOKA /KUWA NA WADUDU.
>>>Chukua magome yake ya ndani changanya na ubani kidogo chemsha,kisha tumia kwa kusukutua na kutema,fanya hivyo mara kadhaa kwa muda wa siku tatu hadi tano,asubuhi na jioni.inshaallah tatizo litakwisha.
12.KUTIBU CHANGO LA UZAZI.
>>>Chukua mzizi wa muembe kisha chemsha alafu kunywa maji hayo kikombe kimoja asubuhi ,mchana na jioni kwa muda wa siku tano hadi saba.
13.KUTOKWA NA MAJI MENGI UKENI.
>>>Chukua kokwa la embe lisage kisha anika unga wake,kisha unga huo utautumia kwa kunawia na maji ya vuguvugu sehemu za siri,asubuhi na jioni.
14.KUMTIBU MWANAMKE ALIYELOGWA KUZIONA DAMU ZAKE KWA MUDA MREFU.AU MWANAUME KUTOSIMAMISHA UUME WAKE.
>>>Chukua magome ya ndani ya mti huo,changanya na kitunguu BAHARI kisha chemsha pamoja alafu tumia kwa kunywa maji hayo asubuhi na jioni kikombe kimoja.Tumia dawa hiyo kwa muda wa siku tatu hadi saba inshaallah tatizo hilo litakwisha.
15.KUMTIBU MTOTO ALIYELEGEA MWILI.(KUBEMENDWA)
>>>Chukua magome ya mti wa muembe kisha chemsha alafu pooza kisha muogeshee mtoto huyo,asubuhi na jioni kwa muda wa siku tano hadi saba inshaallah tatizo litakwisha.
Unaweza kutembelea mitandao yangu ya kijamii kwa ajiri ya kujifunza tiba mbalimbali kupitia Dua mbalimbali,mitishamba na matunda.
Facebook-Tiba facts
Youtube-tibafacts online tv
Instagramu-Ustadh.bashir/@tibafacts
Pia unaweza kujipatia vitabu vyangu vinavyofundisha Elimu ya tiba ukiwa nchi yoyote dunia tunakutumia kwa njia ya mtandao.
1.MAAJABU YA MITISHAMBA KATIKA KUTIBU MARADHI YA KIJINI NA UCHAWI, No.1
Kwa shilingi 7000/= za kitanzania
2.MAAJABU YA MITISHAMBA KATIKA KUTIBU MARADHI YA KIJINI NA UCHAWI,No.2
Kwa shilingi 10000/=
3.TIBA MBADALA KWA MAGINJWA YA KIBAIOLOJIA.
Kwa shilingi 10000/=
4.MAAJABU YA QUR'AN KATIKA KUTIBU MARADHI NA KUONDOSHA SHIDA MBALIMBALI.
Kwa shilingi 12000/=
5.UTUKUFU WA MAJINA 28 YA BARHATIH NA KAZI ZAKE.
Kwa shilingi 15000/=
vitabu vyote unaweza kutumiwa kwa njia ya mtandao ukiwa nchi yoyote duniani.
Wasiliana nami kwa
Sim.+255757455646
au
+255672410104
Namba zote zinapatikana whatsApp