AINA ZA MAJINI NA MUONEKANO WAO NDOTONI.
Katika njia ambayo yatakiwa tabibu (mganga) ajue ni kufahamu aina za majini kutokana na muonekano wao ndotoni baada ya kumuuliza mgonjwa na kujulishwa namna anavyoota.
Kwa sababu ndoto inayotokana na mwenyezimungu inajulikana na ndoto inayotokana na shetani pia inafahamika.Yapasa tabibu ajue ya kwamba majini wako aina mbalimbali na kila mtu atapata athari kwa mujibu wa jini aliyemuingia na ndio sababu ya kuwa majini wanavitimbi mbalimbali na vingi sana kwa kuwa kwao aina nyingi.
Endapo tabibu atajua namna ya vitimbi vyao ambavyo kila uchao ni vyenye kuongezeka kwa sababu nao pia wanakizazi kipya kiletacho vitimbi vipya ,basi mwanadamu nae yampasa afahamu vizuri ili nae ajiandae vya kutosha kukabiliana na adui huyo hatari ambae huwadhihirikia watu ndotoni kwa sura za watu mbalimbali na mara nyingine wanyama kila namna na wadudu pia kama nitakavyo orodhesha ili upate kufahamu.
SURA YA MWANADAMU.
Jini humjia mwanadamu ndotoni kwa sura ya mtu wa karibu yake au kwa sura ya mtu asiyemjua kabisa basi ieleweke kwamba mara nyingi afanyae hivyo ni jini MAHABA ambaye humjia mtu kwa ajiri ya jimai (kufanya nae ngono) mpaka hufanikiwa kustarehe naye,na endapo mtu mwenyewe atakuwa ni mdhaifu wa kiimani ndivyo huyo jini atakavyoweza kumjia kwa namna za watu mbalimbali na kuzini nae hata mzazi wake au ndugu wa tumbo moja au jamaa wa karibu mno.
Siyo ajabu akamjia aliye ndani ya ndoa kwa sura ya mwenza wake .pia anaweza kujiwa na mtu ndotoni anae mtesa sana na kumtisha huyu hahusiani na mapenzi bali huwa ni jini wa kutumikia uchawi na mara nyingi huonekana katika sura ya kasisi.
** SIMBA.
Baadhi ya watu humuona simba usingizini ambaye huyu ni katika majini wakubwa,yaani kiongozi wa kijij ambae ni mshari na anaweza kuwa muislamu au kafiri.
**NYOKA.
Baadhi ya watu humuota nyoka na mara nyingi huyu ni aina ya jini mtumikia uchawi hasa akiwa nyoka mweusi ,Nae endapo atamuota nyoka ni mwenye mbawa na anaruka basi ni katika aina ya majini warukao angani na miongoni mwa majini wanao wakumba watu chooni hasa wale wanaoingia bila ya kusoma dua.Na endapo atakuwa ni nyoka wa kawaida tu na anatambaa ardhini na siyo mweusi basi ni jini tu wa kawaida hahusiani na uchawi na siyo wa chooni.
**NGAMIA.
Baadhi ya watu humuota ngamia,basi huyu ni aina ya jini ambae huwaingia watu ,tena jini mbaya na ni katika viongozi wa majini lakini kuna utofauti wa muonekano wake.
Endapo mtu anamuota ngamia anamfuata nyuma yake basi ajue huyo ni jini hajamuingia lakini yuko kwenye juhudi za kumuingia na akiona amefanikiwa kumgusa basi atambue moja kwa moja kwamba amemuingia tayari.
**BIBI KIZEE
Ni alama ya kuingiwa na jini mtu huyo bila ya sababu za uchawi ila kutokana na sababu nyingine za kawida zipelekeazo mtu kuingiwa na jini,na huwa ni jini wa kati kwa kati na mwenye umri mrefu na kiwiliwili shupavu.
**MBWA MWITU.
Ni alama kwa muotaji kwamba jini aliyemuingia ni mwenye umbile baya na lakutisha lakini mdhaifu wa hila na vitimbi, pindi tabibu akijua hivyo pindi anapodhihiri kwa mgonjwa na akazungumza kupitia kinywa cha mgonjwa basi ni bora tabibu kujua amekaa sehemu gani akamuadhibu hata kwa kumfinya na akamuamuru kutoka basi hulalamika kwa kudhikika kuliko mwanzo kabla ya kufanya hivyo basi ni kujulisha yeye ni katika majini wa jangwani.
>>BAHARI NA SAMAKI.
Baadhi ya watu huota wako baharini iwe wanaogelea au wanavua samaki au wamezungukwa na maji.Pia huota samaki mara kwa mara,basi nia Alama ya kwamba jinialiyemuingia ni mkazi wa baharini ,chini ya bahari na uwezekano wa kukumbana nae mwanadamu ni mtu mwenye kudumu sana kukaa baharini na ufukweni pia bila ya kumtaja m/mungu na hata wale wanaoenda kuogelea tu
TIBA YAKE.
1.Asomewe mtu huyo suratul Baqara,suratul Yunus,suratul Dukhani Aya za adhabu (hizi tutazitaja huko mbele) na aya zinazoelezea gharika kama watu wa nabii Nuhu,Qaruni,au Firauni na aya znazotaja bahari.
2.Pia asome dua za kujiepusha na khofu na kuangamia na atumie miski pamoja na mafusho ya kunukia na kipindi chote cha matibabu asipende kwenda kuogelea baharini wala kutembeatembea ufukweni.
>>NYANI MKUBWA
Hiini aina pekaee ya jini mtumikia uchawi ambae kwa aliemuingia endapo kama atakuwa ni mwenye kukumbuka mno kisimamo baina yake na mola wake siku yaQiyama basi yeye hutenzeka nguvu na kadri atakavyokuwa mwenye kuombadua na kusoma Quran ndivyo atakavyozidi kudhoofika.
>>NYANI MDOGO
Mara nyingi aina hii ya jini huwa ni katika majini wanaishi majumbani wakila na kunywa pamoja na watu wa nyumba hiyo na kulala pasi na wenyewe kujua.
Mara nyingine hujionyesha ndotoni ni mwenye sura iwakayo kama jua na mara nyingi huwa hawi asi na huwa kati kwa kati na endapo itakuwa hiyo nyumba imehamiwa ni gofu basi hugeuka AFRITI akawa mbabe na ndio sababu ya kutakiwa watu wanapohamia majumbani wafanye kisomo maaluumu kabla ya kuhamia laa sivyo hukutana na mauzauza ikawa nyumba haikaliki hasa ikiwa haijakaliwa na watu siku nyingi.
Endapo watu wa nyumba hiyo watakuwa wema basi nae atakuwa mwema na ni mwenye kuiga tabia za watu wa nyumba akaayo.
Sbabu za kukutana nae mara nyingi na mtu kumuingia ni kuwa nyumba hiyo hatajwi mwenyezimungu ,au kupenda kuvua nguo au kulala uchi bila ya kuomba dua za kinga au kumfanyia jambo la kuudhi jini kama kumkanyaga au kumpiga na jiwe au kumwagia uchafu jini huyo.Pia mtu kupenda maasi na kujitumbukiza kwenye madhambi makubwa na mwisho ni mtu kupenda kujihuzunisha na kulia bila ya sababu.
ALAMA ZAKE.
**Mtu atakapoingiwa na jini wa aina hiyo basi atakuwa ni mwenye kupenda kukasirika na kulia bila sababu na kunyongeka kama mgonjwa ,pia atakuwa ni mwenye khofu na fadhaa kwa jambo hata liwe dogo na nyumbani mwake wataonekana wanyama au wadudu wa ajabu
DAW YAKE.
Asomewe suratul Baqara mtu huyo pamoja na kuisoma ndani ya nyumba kwa lengo la kumfukuza jini pia awe ni mwenye kuleta adhkari katika kila jambo lake na asichelewe kunawa mikono.
>>MBWA
Mwenye kumuota mbwa hasa mweusi basi yajulisha yeye ni jini mtumikia uchawi tena myahudi na akiwa wa rangi ya kijani basi ni mnaswara na inajulisha ni katika majini wakaao chooni na yeye amemvaa kwa kukutana nae njiani akamuudhi kwa kumkanyaga au amemkirihi (kumkera) kwa lolote lile .Na ikiwa anamletea kero za usingizini basi ni kwamba hajamuingia bado mwilini na atakapoanza kumdhuru kiwiliwili basi tayari amekwisha muingia.
Ama jini huyu wa chooni ni mshari inatakiwa watu wahadhari nae kwa kuingia chooni kwa mguu wa kushoto na kutoka kwa mguu wa kulia pamoja na kusoma dua ya kuingia na kutoka pia,wasizungumze wakiwa chooni bila ya dharula tena muhimu ,pia waepuke kuimba na kuita kwa sauti ya juu pamoja na kuitika,wasivue nguo ila kwa kiasi cha haja.Pia wasimwage maji au kuyarusha mbali ila kwa kutamka BISMILLAH hasa wakati wa usiku tena waitamke kwa sauti ya kusikika ,akiwa ni mwenye khofu ni wajibu kwake kumkumbuka mwenyezimungu kila wakati kwa ukubwa wake na uwezo wake juu ya viumbe vyake na asipende kabisa kulia chooni iwe kwa siri au kwa sauti.
ALAMA ZAKE KAMA JINI HUYO AMEMUINGIA MTU.
1.Kupenda mgonjwa kuingia chooni mara kwa mara na kukaa huko muda mrefu.
2.Mtu mwingine huingia chooni na akalala na huku akiwa ni mwenye kujisaidia hasa haja kubwa.
3.Kupenda mgonjwa kuwa mchafu hasa kwa kutokuoga.
4.Kupenda kuingia chooni na kiza.
5.Kukereka asikiapo Quran na Adhana.
6.Kudhihiri mabaka mwilini tena kwa msimu kuwa zaidi na msimu kupungua mithiri ya ukoma.
7.Maumivu kwenye uti wa mgongo na kuhisi maumivu katika sehemu kubwa ya mwili wake.
DAWA YAKE.
1.Mgonjwa asomewe suratul Baqara yote.
2.Suratul Qalami ambayo humuunguza sana.
3.Kuwa msafi mgonjwa wa mwili wake nguo zake na makazi yake.
4.Akiwa mwanamke aache kutoka nyumbani kwake hali ya kuwa anamanukato au amejifukiza manukato na awe hivyo akiwa nyumbani tu.
5.Kwa ujumla achunge adabu za chooni.
Jini huyu miongoni mwa vurugu zake ni kuwapiga watu chooni na kuwatisha na kustarehe nao,kimapenzi kwa kuwarazimisha wakiwa hukohuko chooni na akikataa humpiga mtu huyo.
Dawa yake;
yeyote anaeogopa kuingia chooni kutokana na sababu kama hizi basi atakapo kuingia chooni asome Dua ya kuingia chooni kwa sauti au kabla aanze na kusoma ayatul Qursiyyu mara tatu,suratul Humazah mara saba na suratul Zilzalah mara tatu basi hatoona chochote kwa uwezo wa mwenyezimungu.
>>>NGE
Aina hii ni katika majini wa kawaida na mara nyingine hujibadilisha na mtu akamuona katika umbile la kitoto cha mbwa au wadudu watambaao ardhini lakini pamoja na udhaifu wake huwasumbua matabibu kuzungumza nae kutokana na khofu anayokuwa nayo ikapelekea kumshinda hata kuzungumza.
>>>MAKABURI NA MAITI.
Hii ni aina ya jini wa makaburini ambaye humuingia mtu ikawa ndiyo sababu ya kuota mara kwa mara ndoto za makaburini na maiti,na jini mjeuri na makazi yake ni sehemu zenye makaburi yalio mbali na watu au hukaa kwenye msitu ulio jirani na makaburi.
ALAMA ZAKE.
1.Kudhihiri madoa mekundu au makovu mekundu mwilini kwa lengo la kumharibu kiwiliwili.
2.Kuota mgonjwa anakula chakula cha aina yoyote usiku.
3.Kupenda mgonjwa maeneo ya makaburini,na kukaa faragha yaani kujitenga peke yake na kupenda kwenda majangwani na porini.
4.Mara nyingine jini huyu huwa na tabia ya kushika kiungo kimoja iwe mkono au miguu.
5.Mtu huyo pia atahisi mwili wake unawaka moto mara kwa mara.
6.Pia atakuwa mwenye kuota watu waliokufa na makaburi au hata kuhusika yeye na mambo ya kifo.
SABABU ZA KUMUINGIA MTU JINI HUYO.
1.Sababu za kuingiwa na jini huyu ni mara nyingi mtu kupenda kupaza sauti makaburini bila sababu za msingi.
2.Kuwepo makaburini mara kwa mara bila ya sababu zinazohusiano na makaburi kama kuzika,kupima kaburi na ikawa mtu anapatikana sana eneo hilo kwa sababu zake tu kama wanavyofanya baadhi ya watu kuwa ni maeneo ya kukutana kwa ajili ya zinaa,kuwinda ndege n.k.
3.Kunyanyua sauti makaburini hasa nyakati za usiku hata kama kuita au kuitikia aliyeitwa.
4.Kupita makaburini na ikawa mtu huyo hana habari ya kumkumbuka mwenyezimungu kwa hisia na haleti dua maalumu ya makaburini.
DAWA YAKE.
1.Aliyekumbwa na jini huyo atasomewa suratul Baqara,suratul kauthar,na yatasomewa maji anywe na kuoga.
2.Apende kuwa mwenye kuoga na kujitia manukato hasa(miski)na asipende kulia lia bila sababu ya maana.
3.Awe mwenye kukumbuka adhabu za kaburi na kiama na ajiepushe na ukaidi juu ya sheria za mwenyezimungu inshaallah atapona.
JINI MAHABA VITIMBI VYAKE,ALAMA ZAKE KATIKA NDOTO;
Jini mahaba ni miongoni mwa majini hatari tena mwenye visa vingi kupita kiasi hasa akiwa amemkalia mwanadamu siku nyingi.
Mwenye jini mahaba anaweza kukosa kuolewa au kuoa kwa muda mrefu au kushindikana hilo maisha yake yote.
Kazi ya jini mahaba ni kuvuruga mipango ya ndoa au ndoa iliyokuwa teyari.Jini mahaba anaweza kuvuruga shughuri za mtu aliyemtawala hasa mwanamme ili ashindwe kuoa na siku zote abaki kusema tu mambo hayajakaa sawa nitaoa tu.Jini mahaba humfanya mwanamke kutopenda kuolewa.Jini mahaba humfanya mwanamke kutotakwa na wanaume kwa kumuoa ,jini mahaba humsababishia mwanamke aliyeposwa kughairi bila ya sababu za msingi au mwanaume aliyeposa kughairi kwa kuletewa ndoto za vitisho na shetani vya aliyemposa akidai anayetaka kumuoa ni mke wake na akimuoa atadhurika.
Jini mahaba humfanya mume kutoweza kumuingilia mwanamke au kukosa hamu ya tendo hilo .Mwanamke nae huenda akajisikia maumivu pamoja na kutokuwa na hamu ya tendo hilo .Inawezekana mwanamke asisikie ladha ya jimai na mume wake lakini akiingiliwa ndotoni na huyo jini mahaba husikia starehe kama kawaida.Hali hii inapelekea mwanamke kutomthamini mumewe kwa kuwa haoni raha tendo la ndoa.Mwanaume anaweza kupoteza nguvu za kiume lakini ajabu ndotoni hazipotei na atamaliza haja zake zote.
Jini mahaba mwanaume anapenda kulawiti na mwanamke anapenda kulawitiwa.Mwenye jini mahaba kulawiti ama kulawitiwa siyo ajabu ndotoni na atahisi starehe ya jambo hilo na siyo ajabu ikampelekea kulifanya na binadamu wenzake kutokana na hali hiyo,jini mahaba huwa na mapenzi na mtu wake kama ilivyo binadamu kwa binadamu.
Hali hii humfanya jini mahaba awe mbishi kutoka pindi anaposomewa Ruqya.Anaweza kusomewa na akatoka lakini siyo ajabu kurudi tena kwa vile amependa.Kama tunavyofahamu mapenzi jinsi mapenzi yanavyoathiri moyo basi jini mahaba nae huathirika kwayo,akazisikia aya zote lakini akasema "simuachi nitafia palepale kwa jinsi nilivyompenda.
>>SABABU ZA MTU KUINGIWA NA JINI HUYU.
1.Mtu kuvaa nguo ndani mwake bila ya kusoma chochote (dua).
2.kusimama au kukaa nje mwanamke akiwa amevaa mavazi yasiyomsitiri vizuri ikawa watu wanapita wanamuona na kumtamani,basi na majini pia wanamuona na ndiyo sababu ya kumuingia ,na siyo tu kukaa barazani hata mwenye kujitembeza akiwa hivyo.
3.Kulala usiku akiwa mume au mke hasa wakati wa joto bila ya kuvaa kabisa nguo au kuvaa nguo hafifu mno na ikawa mtu huyo hajasoma chochote wakati wa kulala.
4.Kuingia chooni na kutoka pia bila ya kusoma chochote (dua) hasa ya kuingia.
5.Kufanya tendo la ndoa bila ya kuomba dua kabla yake.
NDOTO ZAKE.
Mwenye kuingiwa na jini huyu atakuwa ni mwenye kuota sana awe mume au mke yuko katika tendo la ndoa.
1.Huenda mwanaume akamuingilia mkewe na akatosheka kabisa basi akilala ataota anafanya tendo la ndoa hilo basi hiyo ni dalili ya kwamba yeye ana mke wa kijini anajamiiana nae.
2.Au kinyume na hivyo ni kwamba ni kwamba mume atamuingilia mke wake na baada ya hapo ataota anamuingilia huyohuyo mke wake.
DAWA YAKE.
Dawa ya jini huyu ni miongoni mwa tabu wanazopata matabibu wa ruqya kwa sababu huwa amemng'ang'ania vilivyo lakini huondoka kwa uwezo wake mwenyezimungu.Ni wachache wanaondoka kwa kukinai na kufahamu au kusilimu na kutoka kwa kumtii mwenyezimungu.
Njia ya kwanza ni mgonjwa kusomewa Ruqya (kisomo cha qurani) Suratul
1.Baqara yote,suratul suratul Nnur na aya za vitisho na aya zinazoelezea msaada wa mwenyezimungu na aya zinazozungumzia kupenda kwa ajiri ya mwenyezimungu nazo ni
Suratul Hujurati aya ya 7
Suratul Alqaswaswi aya ya 56
Suratul Al imrani aya ya 31
Suratul Al muntahinah aya ya 8
Suratul Swaaf aya ya 4
suratul Al hashri 9 na zingine tutazitaja huko mbele.pia mgonjwa kutumia manukato hasa miski kwa sababu majini mengi huchukia harufu nzuri hasa jini wa mapenzi na namna ya kutumia ni kupakaa kila tundu la mwili wake kwapembeni kidogo kwa kuanzia mdomoni,puani,masikioni,tupu ya mbele,na tupu ya nyuma,pamoja na ncha za vidole vyote vya mikononi na miguuni na kunyunyiza kitandani na nguo ya kujifunika ndipo alale na atafuata utaratibu huu kwa siku therathini na mbili na apendelee kutia manukato mwili wake aendapo msikitini (kupaka miski)
Unaweza kutembelea mitandao yangu ya kijamii kwa ajiri ya kujifunza tiba mbalimbali kupitia Dua mbalimbali,mitishamba na matunda.
Facebook-Tiba facts
Youtube-tibafacts online tv
Instagramu-Ustadh.bashir/@tibafacts
Pia unaweza kujipatia vitabu vyangu vinavyofundisha Elimu ya tiba ukiwa nchi yoyote dunia tunakutumia kwa njia ya mtandao.
1.MAAJABU YA MITISHAMBA KATIKA KUTIBU MARADHI YA KIJINI NA UCHAWI, No.1
Kwa shilingi 7000/= za kitanzania
2.MAAJABU YA MITISHAMBA KATIKA KUTIBU MARADHI YA KIJINI NA UCHAWI,No.2
Kwa shilingi 10000/=
3.TIBA MBADALA KWA MAGINJWA YA KIBAIOLOJIA.
Kwa shilingi 10000/=
4.MAAJABU YA QUR'AN KATIKA KUTIBU MARADHI NA KUONDOSHA SHIDA MBALIMBALI.
Kwa shilingi 12000/=
5.UTUKUFU WA MAJINA 28 YA BARHATIH NA KAZI ZAKE.
Kwa shilingi 15000/=
vitabu vyote unaweza kutumiwa kwa njia ya mtandao ukiwa nchi yoyote duniani.
Wasiliana nami kwa
Sim.+255757455646
au
+255672410104
Namba zote zinapatikana whatsApp