MASHERTI KWA MSOMAJI WA RUQYA


Yeyote mwenye kufanya ruqya (kisomo cha quran) lazima awe mtu mwenye kujiweka mbali na maasi na awe ni mwenye kutenda mema.

   Ashikamane sawasawa na sunna za mtume (s.a.w) apende kutoa sadaka ,apende kutoa dawa kuhusu athari za majini na mashetani duniani na akhera kwa wagonjwa wake na watu wengine,asichanganye haki na batili ,asipende porojo,na awe mchamungu,masharti yote anayompa mgonjwa kwanza yeye mwenyewe ayatekeleze kwa asilimia kubwa ,asijione mjuzi bali ategemee msaada wa mwenyezimungu  pamoja na kutaka ushauri .Ajikinge na maasi yote kwani ametangaza vita na viumbe waliomzidi uwezo na asiowaona.

   Pia atambue majini wote wanaotoka bila ya kusilimu huwa ni maadui zake na wanaweza kumfatilia nyendo zake ili walipize kisasi takribani miezi mitatu mfululizo  baada ya kutolewa.

           MASHARTI KWA MSOMEWA RUQYA;

   Mwenye kusomewa Ruqya ni lazima adumu kwenye masharti atakayopewa na msomaji ruqya na akiyashika atakuwa mwenye kufanikiwa na asipoyashika hafanikiwi.kinachotakiwa aeleweshwe kwanza maana ya kupewa hayo masharti isije akaona amebebeshwa mzigo tu na hatimae akapuuza .Kwanza aambiwe sababu za mtu kuingiwa na shetani nazo ni,

  1.Kumfanyia ujeuri shetani kama kumpiga bila ya kudhamiria au kumtemea mate nae akakuingia kwa kulipiza kisasi .

  2.Kuingiwa na shetani kwa kurogwa kwani watumikiao uchawi ni mashetani wa kijini.

  3.Kupenda maasi  nae akaona huyu ni mwenzangu tu inafaa kuishi nae pamoja.

  4.Au shetani wa kijini kumuingia  mtu kwa niaba ya kuzini nae.kwahiyo mwanamke wa kijini atamwingia mwanamme wa kibinadamu na mwanamme wa kijini atamuingia mwanamke wa kibinadamu ili wafanye zinaa.

  Pamoja na sababu  hizo zote endapo mtu atajikinga vilivyo  kwa mola wake hawezi kuingiwa na shetani wa kijini kwa namna hizo zote nne  kutokana na huo ulinzi ,na ikitokezea akaingiwa basi itakuwa imepangwa tu iwe hivyo.

    Kwa maelezo hayo mgonjwa atatambua sababu ya kuingiwa na huyo jini kama ni uzembe wake tu  uliomfikishia hali hiyo na ataelewa umuhimu wa kuishi huku akifuata mafundisho ya kiislamu ya kujikinga na shari mbalimbali ikiwemo hao majini.

   Jambo  jingine mgonjwa ni lazima atambue ya kwamba kudumu kwenye masharti ni muhimu kwake,kwa vile anaposomewa Ruqya huyo shetani hukimbia na baada ya kumalizika hiyo ruqya shetani bado hutamani kurudi kwa mtu wake tena endapo hajaondoka kabisa .

   Basi huyo mgonjwa kama akishika masharti sawasawa  hawezi kudhuriwa tena kwa urahisi ,hali hii itaanza kumkatisha tamaa shetani ,na kama hafuati masharti shetani  itakuwa siyo vigumu kwake kumrudia tena na atakuwa mwenye kulipiza kisasi  na mgonjwa atateseka nae hataondoka.

   Vilevile hayo masharti huwa yanamuumiza shetani kwa vile ni kinga ya kitabia ambayo hutakiwa awe nayo mgonjwa(tabia njema) pamoja na dua mbalimali ambazo atasoma kila asubuhi na jioni.

Yeyote mwenye kufanya ruqya (kisomo cha quran) lazima awe mtu mwenye kujiweka mbali na maasi na awe ni mwenye kutenda mema.

   Ashikamane sawasawa na sunna za mtume (s.a.w) apende kutoa sadaka ,apende kutoa dawa kuhusu athari za majini na mashetani duniani na akhera kwa wagonjwa wake na watu wengine,asichanganye haki na batili ,asipende porojo,na awe mchamungu,masharti yote anayompa mgonjwa kwanza yeye mwenyewe ayatekeleze kwa asilimia kubwa ,asijione mjuzi bali ategemee msaada wa mwenyezimungu  pamoja na kutaka ushauri .Ajikinge na maasi yote kwani ametangaza vita na viumbe waliomzidi uwezo na asiowaona.

   Pia atambue majini wote wanaotoka bila ya kusilimu huwa ni maadui zake na wanaweza kumfatilia nyendo zake ili walipize kisasi takribani miezi mitatu mfululizo  baada ya kutolewa.

        SHURTI ZA KUFANIKIWA KISOMO CHA RUQYA.

   >>Masharti ya kisomo cha Ruqya ambayo yakizingatiwa huwa ni sababu ya kufanikiwa na yakipuuzwa huwa ni njia ya kutofanikiwa na tumeyagawanya sehemu tatu nazo ni sehemu inayotumika kusomea,hali anayotakiwa awe mgonjwa na tatu ni hali inayomlazimu tabibu mwenyewe.

             SEHEMU YA KISOMO;

1.Asishiriki mtu ambaye hasomewi akiwa katika hali ya hedhi,nifasi au janaba na mgonjwa husomewa kwa dharura akiwa katika hali hizo endapo amezidiwa na aliyehudhuria bila ya kusomewa atatakiwa awe na udhu.

 2.Ni muhimu kwa watu wanaohudhuria sehemu hiyo kuwa siyo wenye kumuasi mwenyezimungu kwa mwenendo wao pamoja na mapambo yao kama wanaume kuvaa mikufu na hereni au kujipamba kwa dhahabu  au kujichora  mikononi au walevi au wavuta sigara na wanaozungumza habari tofauti na sehemu hiyo kama mpira n.k au kuanzisha mjadala isiyo na maana na haifanani na sehemu hiyo.

  3.Ajiweke tabibu katika hali ya kumpwekesha mwenyezimungu na nia safi na usigeuze sehemu ya porojo.

  4.Awafahamishe watu wake huyo tabibu hapo nyumbani  matokeo ya kazi hiyo ili wawe katika hali ya kujichunga na ushetani isije wakadhurika au kazi yake ikawa ngumu.

5.Aanza tabibu kazi yake akiwa ametwaharika na hiyo sehemu ni twahara na apendelee kuelekea kibra na awatolee mawaidha wagonjwa kabla ya kuwasomea ili wasikie na kuelewa watu na majini wanaowakera  hao wagonjwa .

 6.Mwanamke awe amekuja na maharimu wake anaekubarika kisheria na sio ajiokotee tu mtu au ajitegemee mwenyewe kwa kujiamini tu.

 7.Awatake watu waliopo hapo kutovaa hirizi ,matarasimu na waache kila chenye kumuasi mwenyezimungu.

 8.pasiwepo mahali hapo picha zilizotungikwa akutani za viumbe hai au za kuchonga au midoli, ni sababu ya kutohudhuria malaika.

            MGONJWA MWENYEWE.

1.Awe hasa mgonjwa mwanamke amejisitiri vizuri kwa mavazi ya kiislamu na awe ni mtu mwenye haya.

 2.Aamini Qur'an ni ponyo,na huponya mgonjwa kwa rehma za mwenyezimungu.

 3.Mgonjwa aende kwa tabibu na maharimu wake ili ashuhudie hicho kinachofanyika.

 4.Ikiwa maradhi ni ya kiwili wili ni bora mgonjwa  afanye vipimo kwanza kabla ya kumuendea tabibu.

  5.Ni lazima mgonjwa afuate maelekezo atakayopewa na Tabibu wakati wa tiba na baada ya kupona.

              TIBA YENYEWE.

1.RUQYA iwe ni Qur'an au majina ya mwenyezimungu au sifa zake  pamoja na dua za kuombwa mwenyezimungu pekee.

 2.Kinachosomwa iwe kinaeleweka watu watakapokisikia .

3.TIBA isichanganywe na vitu vyenye kuleta utata kama matalasimu n.k,isipokuwa inajuzu kuandika aya za Quran kwa zafarani na kunywa mgonjwa au kujipakaa au kusomea maji,asali na mafuta ya zeituni au habati sauda akanywa au kujipakaa.

4.Na tiba isichanganyike na kitu haramu kama kuwategemea majini badala ya mwenyezimungu au kutawasali kwa watu waliokufa kwa kuhitaji baraka zao.


  inshaallah tatizo litakwisha.

Unaweza kutembelea mitandao yangu ya kijamii kwa ajiri ya kujifunza tiba mbalimbali kupitia Dua mbalimbali,mitishamba na matunda.

Facebook-Tiba facts

Youtube-tibafacts online tv

Instagramu-Ustadh.bashir/@tibafacts


Pia unaweza kujipatia vitabu vyangu vinavyofundisha Elimu ya tiba ukiwa nchi yoyote dunia tunakutumia kwa njia ya mtandao.

1.MAAJABU YA MITISHAMBA KATIKA KUTIBU MARADHI YA KIJINI NA UCHAWI, No.1

Kwa shilingi 7000/= za kitanzania


2.MAAJABU YA MITISHAMBA KATIKA KUTIBU MARADHI YA KIJINI NA UCHAWI,No.2

Kwa shilingi 10000/=


3.TIBA MBADALA KWA MAGINJWA YA KIBAIOLOJIA.

Kwa shilingi 10000/=

4.MAAJABU YA QUR'AN KATIKA KUTIBU MARADHI NA KUONDOSHA SHIDA MBALIMBALI.

Kwa shilingi 12000/=

5.UTUKUFU WA MAJINA 28 YA BARHATIH NA KAZI ZAKE.

Kwa shilingi 15000/=


vitabu vyote unaweza kutumiwa kwa njia ya mtandao ukiwa nchi yoyote duniani.


Wasiliana nami kwa 

Sim.+255757455646

au

+255672410104


Namba zote zinapatikana whatsApp

    


Previous Post Next Post

Contact Form