Mti wa limao/lemon
Mti wa limao ni miongoni mwa miti yenye maajabu makubwa sana katika ulimwengu wa tiba.Ingawa mti huu umezoeleka na watu wengi wakiutumia katika matumizi ya kawaida,hasa tunda lake likitumika zaidi kama kiungo kinachotumika kwenye mboga,lakini mti huu unamaajabu makubwa ya kusisimua katika ilimwengu wa tiba.miongoni mwa baadhi ya maajabu yake,kupitia mti huu unauwezo wa kumuona mtu anaye kufanyia ubaya,pia ni kinga ya kuwasambalatisha wachawi,na uchawi wao,pia mti huu unauwezo wa kumzuia mtu mbaya asiingie ndani ya nyumba yako,pia unauwezo wa kuondoa uchawi mwilini,kuondoa nuksi au kiza na uchawi wa kumwagiwa katika nyumba yako n.k
Fuatana nami ili tujifunze zaidi baadhi ya faida za mti huu,
1.KUMZUIA MTU MBAYA ASIINGIE NDANI YA NYUMBA AU CHUMBA CHAKO.
Chukua limao likate vipande viwili,kisha tia chumvi ya mawe kidogo katikati ya vipande hivyo kisha chukua kitambaa funga limao hilo.Sehemu utakayo liweka limao hilo mchawi hawezi kuingia kichawi eneo hilo kwa ajiri ya kufanya shughuri za kichawi.
2.UKITAKA KUWAONA WACHAWI NA ULIMWENGU WA KICHAWI;
Chukua malimao saba na sindano za kushonea nguo saba,kisha zichomeke zile shindano saba katika malimao saba kila shindano moja na limao moja,unapozichoma zisitokezee upande wa pili wa limao hilo.kisha zitupe eneo ambalo unakusudia kuwaona wachawi au kuuona ulimwengu wa kichawi mfano mbele ya nyumba yako au barabarani.
Basi endapo kama atapita mtu katika eneo hilo kichawi,au akiwa anafanya shughuri za kichawi eneo hilo hakika utamuona iwe usiku au mchana.
3.UKITAKA KUMUONA MTU ANAYEKUFANYIA UBAYA AU KUKUMBUKA NDOTO UNAZOZIOTA.
Chukua limao kisha likate vipande viwili,halafu unapotaka kwenda kulala koga usafishe mwili wako vizuri kisha chukua kipande kimoja cha limao pakaa maji yake ndani ya viganja vya mikono yako,na kipande kingine pakaa chini ya nyayo za miguu yako.kisha tia nia yako ya kutaka kumuona mtu anayekufanyia ubaya katika ndoto,au kukumbuka jambo lolote utakaloliona ndotoni,basi kwa hakika utaliona jambo hilo ulilokusudia katika ndoto
4.KUMTIBU MTU ALIYELOGWA TUMBO LIKAVIMBA.
Chukua mzizi wa mti wa limao ukate vipande vidogo vidogo,kisha chemsha katika maji kisha tia nia ya kumuondeshea mgonjwa tatizo hilo kisha mpe anywe kikombe kimoja kutwa mara tatu,asubuhu mchana na jioni anywe kikombe kimoja cha chai kwa muda wa siku tatu mfululizo.
5.KUMTIBU MTOTO ANAYEWEWESEKA AU KULIA LIA USIKU.
Kwangua magome ya mti wa mlimao yale ya juu juu kisha yasage upate unga wake.Kisha unga huo changanya na maji unayotumia kumuogeshea mtoto huyo na unga mwingine uchanganye kwenye mafuta yake ya kupaa,uwe unampaka mafuta hayo wakati wa usiku anapokuwa anataka kulala.Inshaalla tatizo la kulialia na kuweweseka usiku litakwisha
6.KUMTULIZA JINI ANAYELETA VURUGU.
>>Endapo kama mgonjwa anasomewa ruqya kisha akawa ni mwenye kufanya vurugu sana kutokana na jini yule baada ya kupanda kichwani basi chukua limao likate vipande viwili kisha mpakae mgonjwa anayesumbuliwa na jini huyo kwenye nyayo zake,inshaallah mgonjwa huyo atakuwa ni mwenye kutulia.
7.KINGA YA KUWASAMBALATISHA WACHAWI NA UCHAWI WAO.
>>Chukua mzizi wa mlimao kisha ukate vipande saba (7) kisha chukua mzizi wa mbaazi ukate vipande saba(7) kisha chukua mzizi wa mnyonyo au mbalika nao ukate vipande saba,kisha chukua chupa tia vipande hivyo vyote kwenye chupa hiyo pia tia mafuta ya ndimu kidogo kwenye chupa hiyo,tia mafuta ya mlihani ndani ya chupa hiyo,tia mafuta ya kitunguu swaumu ndani ya chupa hiyo,tia mafuta ya nyonyo ndani ya chupa hiyo,pia weka unga kidogo wa makata ndani ya chupa hiyo.kisha funga.
Kisha tia nia yako juu ya kuhitaji ulinzi na kinga kwa kumuomba mwenyezimungu.Sehemu ambapo mchanganyiko huo utauweka kwa nia ya kuweka kinga ima ya nyumba au biashara au banda la mifugo n.k,mchawi yeyote akija eneo hilo katika mazingira ya kichawi hakika atapotea.kinga hii inauwezo wa kumsambalatisha mchawi na kumpoteza kabisa.
8.KUMUHAMISHA MCHAWI ENEO LAKO AU NDANI YA NYUMBA YAKO AU KUMZUIA MCHAWI ASIINGIE ENEO LAKO AU KUMZUIA MCHAWI ASIPITE ENEO LAKO.
>>Chukua pilipili kichaa,itwange upate unga wake,chukua maji ya ndulele,kisha chukua maji ya ndimu,kisha chukua maji ya limao,vyote hivyo tia kwenye chupa kisha tia niayako juu ya kuhitaji kinga dhidi ya watu wabaya na wachawi wanaokuja katika eneo lako kukuchezea.Chupa hiyo utaiweka katika mlango wako ndani au nje au katikati ya uwanja wako wa nyumba yako.
Eneo hilo mtu mbaya akija dalili ya kwanza ataanguka na kuanza kuropoka maneno ya ajabu na kuzungumzia nia ya jambo lililomleta hapo kwako.
9.KUONDOA NUKSI /KIZA NA UCHAWI WA KUMWAGIWA KATIKA BIASHARA YAKO AU NYUMBA YAKO.
>>>Chukua limao kamulia kwenye maji changanya na chumvi ya mawe kiasi cha gao la mkono mmoja,kisha iache chumvi iyeyuke vizuri kisha pigia deki au nyunyizia maji hayo katika eneo lako.Inshaallah uchawi huo utakuwa umebatilika.
10.KUONDOA UCHAWI MWILINI.
Chukua limao kamulia kwenye maji kisha changanya na chumvi ya mawe kidogo,kisha koga maji hayo kwa nia ya kuondosha uchawi mwilini mwako.Inshaallah uchawi huo utakua umebatilika kwa uwezo wa mwenyezimungu.
MTI WA LIMAO.
11.KUTIBU TATIZO LA MDOMO KUTOA HARUFU MBAYA.
>>Chukua maji ya limao changanya na maji kidogo tumia kwa kupigia mswaki ,fululiza asubuhi na jioni angalau wiki moja.Inshaallah tatizo litakwisha.
12.KUUPA PAWA (NGUVU ) MWILI KITIBA.
>>Chukua kivumbasi pondaponda kisha changanya na maji ya limao kisha tumia kwa kuoga maji hayo ,Inshaallah mwili wako utakuwa na pawa kubwa.
13.KUTIBU VITU VINAVYOTEMBEA MWILINI VINAVYOTOKANA NA UCHAWI.
Chukua mzizi wa limao,mzizi wa ndimu,na mzizi wa mbaazi kisha funga mizizi hiyo kisha weka kwenye chombo chemsha,kisha maji hayo atatumia kwa kunywa kikombe kimoja asubuhi mchana na jioni kwa muda wa wiki moja mfululizo.
Pia atachukua majani ya ndimu,majani ya mlimao,majani ya mbaazi na majani ya kivumbasi kisha yakaushe kisha yatwange upate unga wake.Unga huo tumia kuchanganya katika chai yaani yafanye kama ndio majani yako ya chai.tumia hivyo kwa mda wa wiki mbili au zaidi kupata matokeo mazuri.
14.KUTIBU KIUNGULIA.
>> Chukua majani ya limao kisha changanya katika chai kisha chemsha pamjoja.Tumia kwa kunywa asubuh grasi moja na jioni gasi
15.KUTIBU TATIZO LA KUPOOZA MWILINI.
>>Chukua majani ya ndimu na majani ya limao,kisha chukua maganda ya ndimu na maganda ya limao kisha viunguze alafu upate ungaa wake.Unga huo utatumia kuchanganya na dawa zifuatazi
1.Kitunguu swaumu kipondeponde.
2.Mafuta ya ndimu,
3 Mafuta ya Zaituni
4.Mafuta ya kitunguu swaumu,
5.Mafuta ya nazi
6.HALIMITI
7.TUFANI JINI
8.KALAFUU MAITI
9.HALITITI
10.KIBELITI UPELE
11PILIPILI MANGA
Dawa zote hizo uzisage ziwe katika mfano wa unga unga,pia dawa hizo na mafuta hayo yanapatikana katika maduka yanayouza dawa za kisunna .
Changanya vitu vyote vilivyo hapo juu kisha weka na ule unga uliouunguza katika mchanganyiko wa mafuta na vitu hivyo.kisha tumia kwa kumchua mgonjwa asubuhi na jioni kwa muda wa siku 30.Inshaallah tatizo litaondoka .
Unaweza kutembelea mitandao yangu ya kijamii kwa ajiri ya kujifunza tiba mbalimbali kupitia Dua mbalimbali,mitishamba na matunda.
Facebook-Tiba facts
Youtube-tibafacts online tv
Instagramu-Ustadh.bashir/@tibafacts
Pia unaweza kujipatia vitabu vyangu vinavyofundisha Elimu ya tiba ukiwa nchi yoyote dunia tunakutumia kwa njia ya mtandao.
1.MAAJABU YA MITISHAMBA KATIKA KUTIBU MARADHI YA KIJINI NA UVHAWI, No.1
Kwa shilingi 7000/= za kitanzania
2.MAAJABU YA MITISHAMBA KATIKA KUTIBU MARADHI YA KIJINI NA UCHAWI,No.2
Kwa shilingi 10000/=
3.TIBA MBADALA KWA MAGINJWA YA KIBAIOLOJIA.
Kwa shilingi 10000/=
4.MAAJABU YA QUR'AN KATIKA KUTIBU MARADHI NA KUONDOSHA SHIDA MBALIMBALI.
Kwa shilingi 12000/=
5.UTUKUFU WA MAJINA 28 YA BARHATIH NA KAZI ZAKE.
Kwa shilingi 15000/=
vitabu vyote unaweza kutumiwa kwa njia ya mtandao ukiwa nchi yoyote duniani.
Wasiliana nami kwa
Sim.+255757455646
au
+255672410104
Namba zote zinapatikana whatsApp.
![]() |